NYOTA NDOGO: NIACHENI NA NDOA YANGU

0
956

NAIROBI, KENYA


MSANII wa muziki nchini Kenya, Nyota Ndogo, ametumia akaunti yake ya Instagram na kuwaambia maadui zake kwamba, wamuache na ndoa yake.

Msanii huyo amefanikiwa kufunga ndoa na mpenzi wake raia wa nchini Denmark, Henning Nielsen, lakini baadhi ya maadui zake wameanza kumshambulia kupitia mitandao ya kijamii kwa kudai kuwa, mume wa msanii huyo ni mzee.

“Ukizeeka bila bwana utaambiwa mwanamke hadi sasa hajaolewa anangoja nini? Mungu akikupa mwanamume utaanza kusikia ameolewa na babu au amefuata fedha.

“Naomba niweke wazi kwamba, nimeolewa na mzungu wangu bila kujali umri wake na sijafuata fedha, kwa kuwa hata yeye amenikuta nikiwa na fedha zangu, hivyo naomba niacheni na ndoa yangu,” aliandika Nyota Ndogo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here