Nyota Kilimanjaro Queens aita mashabiki Chamanzi

0
744

GLORY MLAY –DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Kilimanjaro Queens, Fatuma Mustapha amewataka mashabiki wa kikosi hicho wajitokeze kwa wingi kwenye michuano ya Cecafa inayotarajiwa kuanza Jumamosi hapa nchini.

Michuano hiyo ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) inatarajiwa kuanza Jumamosi hadi 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Fatuma alisema mashabiki wanapaswa kuwa silaha ya kwanza kumalizia burudani kila watakaposhuka dimbani na wapinzani wao Sudan katika mchezo wa kwanza.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona namna tutakavyofanya kweli mbele ya Sudan kwani tumejipanga na tupo vizuri, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti na tutatoa burudani ya kutosha.

“Kilimanjaro inapofanya vizuri ni Tanzania kwa ujumla, kama wachezaji tunajua majukumu yetu ya kufanya uwanjani kwani mwalimu ameshafanya kazi yake, nina imani tutashinda,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here