25.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 31, 2023

Contact us: [email protected]

Nyoni atoa siri penalti ya kwanza Stars

Theresia Gaper -Dar es salaam

NAHODHA msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Erasto Nyoni, amesema alichagua kupiga penalti ya kwanza katika mchezo na Kenya ili kuwapa moyo wenzake.

Katika mchezo huo wa marudiano wa kufuzu michuano za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN), Stars ilishinda iliibuka kidedea  ikishinda kwa penalty 4-1, hivyo kufanikiwa kusonga mbele.

 Mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Kasarani, Kenya, waliingia katika penalti baada ya kutoka suluhu ndani ya dakika 90 na ule wa kwanza uliopigwa Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANI, Nyoni, alisema Watanzani wanatakiwa kuendelea kuisapoti timu yao ili ifanye vizuri  katika hatua inayofuata.

“Nimefurahi sana timu yetu kusonga mbele, hali hii imezidi kutupa morali ya juu, ujue nilijitoa kwenda kupiga penalti ya kwanza ili kuwatoa hofu wadogo zangu na ilifanikiwa kwani walipiga penalti zote bila wasiwasi,”alisema.

Alisema hawajaishia hapo, wataendelea kupambana  katika mechi zijazo na kufanya vizuri zaidi.

Naye John Bocco, alisema ushindi waliopata ni kwa Watanzania wote, hivyo wanajipanga kwa mechi inayokuja dhidi ya Sudan waweze kufanya vizuri.

“Tunashukuru Watanzania waliweza kujitokeza katika mchezo huu japo walikuwa wachache lakini walishangilia kwa nguvu zote na kutupa morali ya kupata ushindi na kusonga mbele,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,315FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles