24.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Nyihita ateuliwa kuwa Mlezi wa Vijana Mkoa wa Mara

Na Mwandisi Wetu, Mara

Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Taasisi ya kusaidia vijana sekta ya kilimo cha umwagiliaji imemsimika rasmi muwekezaji wa kiwanda cha kuchakata na kusindika mafuta ya Alizeti wilayani Rorya mkoani Mara, Mkurugenzi wa kampuni ya Nyihita sunyfolwer, Wilfred Nyihita kwa lengo la kuongeza uzalishai mali utakao saidia kukabiliana na upungufu mkubwa wa chakula zaidi ya tani 217,000 ikilinganishwa na uzalishaji uliopo kwa sasa wa tani laki sita wakati mahitaji ya mkoa ni zaidi ya laki nane kwa mwaka.

Hafla ya uzinduzi wa Taasisi hiyo mkoani Mara na kumsimika Mlezi wa Vijana kupitia Yaasisi Tanzania Youth Agro Irrigation Development Network Programme imefanyika Septemba16, 2023 mjini Musoma katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mara ambapo Nyihita na Uongozi wa Taasisi hiyo wametiliana saini ya makubaliano kwa lengo la utekelezaji utakao anza mwaka huu 2023.

Hafla hiyo imehudhuriwa na wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya, Maafisa Kilimo,viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, Wanasiasa, wakulima na taasisi za kijamii.

Akisoma Taarifa kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, Afisa Kilimo Mkoa wa Mara, Lazaro Butilikwa amesema jitihada za Serikali ni kuhakikisha vijana wanapata mitaji ya kilimo kupitia mikopo ya asilimia nne inayotolewa na halmashauri za wilaya iliwemo kupewa Ardhi ya kutosha kwa ajili ya kuanzisha mashamba darasa kwenye maeneo yao.

Akizungumza baada ya kusimikwa rasmi kuwa mlezi wa Vijana Mkoa wa Mara Nyihita amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha mpango wa programu ya kuwajengea uwezo vijana katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (BBT) ili waweze kuzalisha kwa tija kutokana na teknorojia za kisasa ili kusaidia Taifa kupata chakula cha kutosha na ziada ya kuuza nje ya nchi hali itakayokuza pato la Taifa.

“Mkoa wa Mara unahitaji kuwa na vijana wenye mtazamo na maono yenye tija ili kuenzi muasisi wa taifa hayati Mwl Julias Nyerere ambaye alikomboa taifa kwa wakoloni na kuhimiza jamii kuwa kilimo ni uti wa mgongo, hivyo vijana wanatakiwa kutumia fursa zilizopo kwa kujipatia kipato kupitia kilimo cha kisasa kwa lengo la kujikwamua kwenye lindi la umasikini,”amesema.

Nyihita ameihakikishia Serikali Kuu kusimamia kikamilifu mpango wa kuwezesha vijana kuimarisha kilimo chenye tija ili baada ya muda mfupi Mkoa wa mara uonyeshe mapinduzi ya kijani kuwa wa mfano kati ya mikoa ya kanda ya ziwa kwa kuwa vijana wengi wamesoma na wamepania kujiajili kupitia kilimo chenye tija ili kuondokana na tatizo la upungufu wa chakula zaidi ya laki mbili kila mwaka

Baadhi ya Vijana wa Mkoa wa Mara wameishukuru Serikali kuanzisha programu hiyo ambayo itasaidia kuwakomboa vijana kupata ajira kupitia kilimo huku wengine wakipongeza ofisi ya waziri mkuu kumteua mkurugenzi wa Kiwanda cha Kuchakata na kusindika Alizeti wilaya ya Rorya, Wilfred Nyihita ambaye amekuwa chachu kwa vijana kuelimisha kilimo ikiwemo kugawa mbegu za alizeti bure kwa wakulima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles