32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Nyerere atawala mkutano SADC

Abasi Shabani (SJMC), Dar es Salaam

Rais Dk. John Magufuli amefunga Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ulioanza jana Jumamosi Agosti 17 na kumalizika leo huku akimtaja Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere kama mtu aliyejitolea maisha yake katika kusaidia wengine.

Akihitimisha mkutano huo leo Agosti 18, jijini Dar es Salaam, Rais Dk. Magufuli amesema suala la kutoa huwa ni gumu sana kwa watu wengine, ambapo wako wanaojitolea kutoa figo wako wanaojitolea maisha yao kwa ajili ya kuokoa watu wengine.

Amesema Baba wa Taifa aliamua kutoa maisha yake kwa wananchi wake na kwa taifa lake na mataifa mengine.

“Kule Mazimbu Morogoro ilikuwa sehemu ya ANC na Dakawa pia, ninashukuru Rais Cyril Ramaphosa (Rais wa Afrika Kusini) alikwenda pale Mazimbu na akashuhudia makaburi zaidi ya 76 ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini na majina yote ni ya makabila ni ya Afrika Kusini.

“Na kikubwa alichokiona ni mabinti wakubwa ambao wamelitafuta kaburi la baba yao kwa muda mrefu hawakujua kama alizikwa Mazimbu, ilikuwa uchungu mkubwa.

“Lakini hii inaonyesha jinsi gani baba huyu aliyeitwa Julius Nyerere alivyokuwa akijitoa hata kwa kuisababishia nchi yake na watu wake wapate shida ili nchi nyingine ziweze kukombolewa.

“Lakini historia ya Baba wa Taifa, haiishii hapo, mwaka 1975 Jeshi la Tanzania lilikwenda Shelisheli kuzima mapinduzi, nakumbuka Brigedia Jenerali Ngwilizi alikaa kwa muda kadhaa akiwa rais baada ya mapinduzi hayo.

“Lakini baada ya hapo Tanzania imeendelea kushiriki misheni mbalimbali ikiwemo Comoro na DRC (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo), lakini haya yote yalitokana na baba mmoja aliyelipenda taifa hili na akawapenda majirani zake,” amesema Rais Dk. Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles