29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

NYAMBIZI YA MAREKANI YAWASILI KOREA KUSINI

SEOUL, KOREA KUSINI


WAKATI Korea Kaskazini ikifanya zoezi kubwa la kijeshi huku kukiwa na wasiwasi itaendesha jaribio jingine la kombora au silaha za nyuklia, nyambizi ya Jeshi la Marekani imewasili Korea Kusini.

Nyambizi hiyo, USS Michigan yenye uwezo wa kushambulia kwa makombora, itajiunga na kundi jingine la meli za kivita zinazoelekea eneo hilo, zikiongozwa na Carl Vinson, ambayo hubeba ndege.

Korea Kaskazini iliadhimisha miaka 85 tangu kuanzishwa kwa jeshi lake jana, ambapo ilifanya zoezi kubwa la kijeshi likihusisha ufyatuaji wa risasi.

Miaka ya nyuma, imekuwa ikiadhimisha siku hiyo kwa kuzindua makombora na silaha nyingine.

Wasiwasi umeongezeka wiki za karibuni kutokana na taifa hilo na Marekani kujibizana vikali na kutoleana vitisho.

Wakati hayo yakijiri, katika tukio ambalo si la kawaida, Bunge la Seneti nchini Marekani limealikwa kwa kikao cha kupewa taarifa kuhusu Korea Kaskazini Ikulu mjini Washington leo.

Nyambizi ya USS Michigan hutumia nguvu za nyuklia na hubeba makombora aina ya 154 Tomahawk na wanajeshi 60 pamoja na nyambizi nyingine ndogo, gazeti la Korea Kusini la Chosun Ilbo limeripoti.

Meli hiyo inatarajiwa kushiriki kwenye mazoezi ya kijeshi pamoja na kundi la meli zinazoongozwa na Carl Vinson, ambalo lilitumwa eneo hilo kuonyesha ubabe wa kijeshi wa Marekani.

Awali meli hizo za kivita zilizua utata baada ya sintofahamu ya mahali zinakoelekea.

Pyongyang ilikerwa na kutumwa kwa meli hiyo na imetishia kuizamisha kwa ‘shambulio moja kubwa’ dhidi ya ilichosema ni uchokozi wa Marekani.

Wakati huo huo, Rais Xi Jinping, akizungumza kwa njia ya simu na Rais Trump jana, alizihimiza pande zote kuvumiliana na kujiepusha na vitendo ambavyo vinaweza vikaongeza wasiwasi zaidi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles