29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Nyamagana waja na Samia CUP

Na Sheila Katikula, Mwanza

Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza imezindua bonanza la mashindano ya michezo yanayofahamika kwa jina la SAMIA CUP kama sehemu ya kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi na kuunga mkono juhudi za Rais wa Tanzania, Sami Suluhu.

Bonanza hilo la michezo limezinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dk.Philis Nyimbi ambapo linatarajiwa  kufaanyika kwenye Uwanja wa michezo wa Nyamagana uliopo jijini Mwanza.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dk.Nyimbi alisema bonanza hilo ni jukwaa kubwa kuitanganza wilaya ya Nyamagana hivyi ni vyema wachezaji wakawa na nidhamu ili kuendeleza na kuonyesha vipaji vyao pamoja na kutoa burudani kwa watazamaji. 

Kwa upande wake Katibu Wa Chama cha Mpira Wilaya ya Nyamagana  (NDFA) ambao ndiyo waratibu na waandaaji  wa bonanza hilo, Kurwijila Malima alisema mpaka sasa timu 11za mkoani hapa  zitashiriki bonanza hilo.

Malima aliongeza kuwa, miongoni mwa timu hizo pia zimepewa nafasi timu za  Mwanza Veteran na timu ya magereza kushiriki bonanza ili kuongeza chachu ya ushirikiano baina ya makundi mbalimbali ndani ya jamii ambapo yimu hizo zilicheza mchezo wa ufunguzili

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles