26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

NUSU WAGONJWA WA FISTULA HUKOSA MATIBABU

JOHANES RESPICHIUS

-DAR ES SALAAM

KUTOKANA na upungufu wa madaktari bingwa wa ugonjwa wa fistula, imeelezwa kuwa nusu ya wagonjwa hawapati matibabu.

Hayo yalisemwa na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Fistula kutoka Hospitali ya CCBRT, Dk. James Chapa, katika semina ya waandishi ya habari iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) kwa kushirikiana na Hospitali ya CCBRT na Shirika la Utafiti wa Tiba na Afya barani Afrika (AMREF).

Dk. James alisema kila mwaka wanawake wanaougua ugonjwa wa fistula ya uzazi ni 3,000, ambapo ni wagonjwa 1,500 hadi 2,000 wanaopatiwa matibabu.

“Nchi za kusini wa Jangwa la Sahara ndizo zinaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi wa fistula ambapo kwa Tanzania pekee inakadiriwa kwa  mwaka ni 3,000, lakini kutokana na uhaba wa madaktari bingwa, ni wagonjwa 1,500 hadi 2,000 wanaopatiwa matibabu.

“Hivyo kutokana na hali hiyo, karibu nusu ya wagonjwa huwa hawapatiwi matibabu ambapo wengine wamekuwa wakipoteza maisha, Mataktari bingwa wa upasuaji wa ugonjwa huu nchi nzima hawazidi 17, ambapo wanalazimika kufanya kazi katika vituo 14 vilivyopo nchini,” alisema Dk. James.

Awali kuelekea Siku ya Maadhimisho ya Fistula Duniani, ambayo hufanyika Mei 3, kila mwaka, Mwakilishi wa UNFPA nchini, Dk Hashina Begum, alisema katika kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi 2016 shirika hilo limeweza kusaidia upasuaji kwa wanawake 85,000 kutoka nchi mbalimbali.

Alisema fistula ni tatizo ambalo kama mama akiwahishwa hospitalini wakati wa uzazi anaweza kupata matibabu na kupona kabisa, tofauti na taarifa zilizokuwa zikienea kuwa ugonjwa huo unatokana na mambo ya kishirikina.

Alisema maadhimisho hayo kwa mwaka huu yatakuwa na kauli mbiu ya ‘Tumaini, Uponyaji na Heshima kwa Mwanamke’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles