Na JUSTIN DAMIAN
KAHAWA ni kinywaji chenye watumiaji wengi kote duniani. Kinywaji hiki kinashikilia nafasi ya pili kwa wingi wa watumiaji baada ya maji duniani. Kibiashara, ni bidhaa namba mbili inayoongoza kwa mauzo baada ya mafuta.
Zao la kahawa lina historia ndefu pamoja na faida nyingi, zikiwamo za kiafya pamoja na za kiuchumi. Wataalamu wa masula ya afya wamekuwa wakiwashauri watu kutumia kinywaji cha kahawa kutokana na faida nyingi wanazoweza kuzipata.
Pamoja na umuhimu wake kiafya, matumizi ya kahawa bado yapo chini sana kwa hapa Tanzania. Kwa mujibu wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB), ni asilimia saba tu ya kahawa inayozalishwa hapa ndiyo inatumika nchini.
Hata hivyo, kwa miaka ya karibuni kumekuwapo na makampuni mbalimbali ambayo yamekuwa yakijitokeza kubuni bidhaa mbalimbali za kahawa, ili kuupa umma hamasa ya kutumia kinywaji hiki.
Jarida la Uchumi na Biashara lilifanikiwa kufanya mazungumzo na mkurugenzi wa Kampuni ya Dar es Salaam Merchant Group, Rayton Kwembe, ambao ni wasambazaji wa kinywaji cha Nuru Coffee Chapchap. Tofauti na kahawa ya kawaida ambayo imezoeleka, Nuru Coffee imekuja na ubunifu wa aina yake, ikiwa na vitu vitatu ndani yake.
Mkurugenzi huyo anasema: “Nuru Coffee Chapchap ni kinywaji kipya nchini Tanzania chenye mchanganyiko wa viungo vitatu, yaani kahawa, maziwa na sukari ndani ya pakiti moja. Ni rahisi kutumia, unachotakiwa kufanya ni kufungua pakiti ya Nuru Coffee Chapchap kisha changanya na maji ya moto kwenye kikombe kidogo cha kahawa,” anaeleza.
Alipoulizwa ni nini kilichowafanya kuja na wazo la kuwa na kinywaji chenye vitu vitatu kwa pamoja, alisema: “Maisha yamebadilika na mambo mengi yanakwenda kwa kasi.
“Kwa kulitambua hilo, tuliona kuwa ingekuwa ni vyema tukaja na bidhaa yenye kumrahisishia mlaji kazi wakati wa kuandaa kinywaji chake. Pia lengo letu ni kumpa mteja thamani zaidi kwa pesa anayotoa, ndiyo maana tukaja na wazo la kuwa na bidhaa yenye viungo vitatu lakini kwa bei ya kimoja.”
Rayton anafafanua kuwa, kinywaji cha Nuru Coffee Chapchap kinaweza kutumiwa na mtu yeyote, ile kwa urahisi, huku akisisitiza kuwa upatikanaji wake pia ni rahisi, kwa kuwa inapatikana katika maduka mitaani na hata supamaketi ndogo na kubwa.
“Nuru Coffee Chapchap inapatikana madukani katika mfuko mkubwa wenye pakiti hamsini na mfuko mdogo wenye pakiti kumi ndani. Bei yake ni shilingi 500 kwa pakiti, hivyo mfuko mkubwa wenye pakiti 50 ni shilingi 25,000 na mdogo wenye pakiti 10 ni shilingi elfu tano,” anasema.
“Unapoamka asubuhi na kufikiria unahitaji kitu gani kwa kufungua kinywa na kukufanya uchangamke wala usihangaike. Fungua pakiti yako ya Nuru Coffee Chapchap kisha changanya na maji ya moto kwenye kikombe kidogo, hapo utakuwa umejipatia vitu vitatu kwa mpigo kwa chapchap, yaani kahawa, maziwa na sukari ndani ya pakiti moja, yaani tatu mara moja.
“Wakati wa mchana ukiwa ofisini umetingwa na kazi nyingi unaweza kutumia kinywaji hiki kwa sababu kitakuburudisha, kukuchangamsha na kukufanya uwe na hali nzuri,” anaeleza.
Mkurugenzi huyo aliwataka Watanzania kutumia kahawa kutokana na umuhimu yake kwa afya zao
“Kahawa ina faida kubwa mwilini, kwani huburudisha mwili, huchangamsha (wakati wowote hujisikia furaha), kufikiri kwa haraka na kutosahau, huongeza uwezo wa ufahamu kiakili.
“Pia kahawa ina faida mbalimbali za kiafya, kwani hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa mbalimbali kama saratani, kisukari, kusahau, kupunguza unene na msongo wa mawazo,” aliongeza.
Faida nyingine za kutumia kahawa ni pamoja na;
Inapunguza kupata kisukari (Diabetes Type 2)
Watumiaji wa kahawa wana uwezo wa kupunguza kasi ya kupata magonjwa ya kisukari. Utafiti uliofanywa na The American Chemical Society unaonyesha kuwa watu wanaokunywa vikombe 4 na zaidi kwa siku, wanapunguza uwezekano wa kupata sukari kwa asilimia 50.
Inachangamsha mwili na ubongo
Mzunguko mzuri wa damu husaidia usafirishwaji wa hewa ya oxygen mwilini na kwenye ubongo. Hii inafanya mtu kuwa na mawazo mazuri na kufanya ubongo ufanye kazi vizuri. Hutoa uchovu wa kazi na ulevi kwa wale wanaokunywa pombe.
Huepusha Kansa ya Ngozi
Japokuwa hakukuwa na ushahidi wa kitaalamu sana, ila kundi la watafiti wakinamama kutoka Brigham na Harvard University walisema wanawake wanaotumia vikombe 3 na zaidi vya kahawa kwa siku wana uwezekano mdogo wa kupata kansa ya ngozi ukilinganisha na wasiotumia kabisa.
Inaimarisha uwezo wa kufikiri
Kwa kuwa kahawa inaongeza msukumo wa damu, inasaidia ufanyaji kazi mzuri wa ubongo, hivyo ni rahisi kufanya vitu kiumakini zaidi kwa kuimarisha afya ya ubongo, kutokusumbuliwa na usahaulifu na kuimarisha uwezo wa kufikiri pia.
Ofisi nyingi huwapatia wafanyakazi wake kinywaji cha kahawa ambacho huweza kutumika muda wowote .