27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Nundu apiga hesabu ubunge Tanga Mjini

OSCAR ASSENGA-TANGA

ALIYEKUWA Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano katika Serikali ya Awamu ya Nne, Omari Nundu ametangaza nia ya kuwania ubunge Jimbo la Tanga Mjini, mwaka 2020 pindi CCM itakapotangaza utaratibu rasmi.

Amesema baada ya chama hicho tawala kutangaza utaratibu rasmi atachukua fomu na kuirudisha ili kuomba ridhaa ya chama hicho.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini Tanga, katika hafla ya kukabidhi vifaa tiba katika Hospitali ya Wilaya vilivyotolewa na wadau wa maendeleo kupitia mitandao ya kijamii ya WhatsApp.

Nundu aliwahi kuwa mbunge wa jimbo hilo mwaka 2010 hadi 2015 alipopigwa mweleka wa kushindwa na Mbunge wa sasa, Mussa Mbaruku (CUF).

“Labda niwaambie kwamba ikifika mwaka 2020 wakati wa kugombea nitachukua fomu, nitazijaza na kugombea, lakini kwa sasa hamtoniona nikigawa fedha kwa watu elfu ishirini ishirini wala futari.

“Nimesikia maneno mtaani yanapita kwamba Nundu anataka kugombea ubunge, niwaambie kwamba ikifika mwaka 2020 wakati ukifika na chama kikitangaza utaratibu wake, nami nitajitosa, lakini si sasa jamani, chama bado hakijasema ndugu zangu,” alisema Nundu.

Alisema katu hawezi kutoa fedha kwa watu ila atashiriki kila hatua katika shughuli za maendeleo ya Jimbo la Tanga na mkoa mzima.

 “Nitasimamia suala la maendeleo mpaka hatua ya mwisho, sasa tuna rais (Dk. John Magufuli) ambaye anasaidia na kusukuma maendeleo kwa kasi kubwa kwani matunda yake yameonekana kwenye sekta mbalimbali,” alisema.

Awali akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Daudi Mayeji, aliwashukuru wote waliochangia vifaa hivyo vya matumizi ya hospitali na kusema sasa watakuwa wanapokea vifaa kwa utaratibu wa kiserikali.

Mayeji alisema kwamba wao Serikali wanapokea misaada yoyote ile hasa isiyo na masharti na wanaingiza kwenye matumizi, kwamba hawana sababu yoyote ya kukataa kitu ambacho kimekuwa kikitolewa na wadau.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles