26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Nuh Mziwanda: Shilole anipige tu! hakuna shida

Nuh na ShiloleNA MWALI IBRAHIM
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Nuh Mziwanda, ametoa kali ya mwaka kwa kudai kwamba kitendo cha kupigwa mara kwa mara na mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, kinampa furaha na ufahamu wa namna anavyopendwa.
“Kwanza kupigwa raha, mpenzi wako asipokupiga hakuonei wivu, mimi nafurahi sana na namtaka anipige tu! kila siku akijisikia, ananidhihirishia kuwa ananipenda,” alisema.
Nuh alisema mengi yamesemwa kutokana na kupigwa kwake mara kwa mara, huku akidai kwamba hilo halina tatizo kwake, kwa kuwa halitaharibu mapenzi yao wanayoamini yatafika mbali.
“Sisi tunawezana na Mungu atusaidie tufikie katika hatua ya ndoa tuliyojiwekea,’’ alimaliza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles