25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

NTS – BOSCH wazindua maonyesho na kituo cha huduma Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya NTS-Bosch inayojihusisha na uuzaji wa zana za umeme, imezindua monyesho na kituo cha huduma jijini Dar es Salaam ikilenga kuwasaidia Watanzania hususan mafunzi wa ndani pamoja na kukuza ajira.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika leo Februari 14, 2023 kilichopo Kamata Cmplex, Kariakoo, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NTS-Bosch, Amin Lakhani amesema kuwa kufunguliwa kwa duka hilo ni mwanzo wa wananchi kupata bidhaa bora na za kuaminika.

Mmoja wa Wafanyakazi wa kampuni hiyo akielezea moja ya bidhaa zinazopatikana kituoni hapo.

“Sisi ni wasambazaji wa zana za nguvu za Bosch tulioidhinishwa na tunaweza kuhudumia zana zote za nguvu za Bosch katika kituo chetu cha huduma kilichoidhinishwa, hivyo leo tumefungua kituo hiki maalumu kwa ajili ya kuwasogezea huduma Watanzania, kwani eneo hili ni sehemu amb ayo kiola mtu anapita kwa ajili ya kutafuta vipuri mbalimbali.

“Sambamba na hayo nibaya kabisa ikwamba hii itasaidia kuchochea ujuzi kwa mafunzi wazawa kupitia wataalamu wetu waliiko hapa, lakini pia itatengeneza ajira kwa Watanzania wenzetu, hivyo niwaombe watu wakitumia kitu chetu hiki kwa ajili ya kupata zana mbalimbali zikiwamo za umeme,” amesema Lakhani. 

Ameongeza kuwa kitengo cha zana za Nguvu cha Bosch GMBH ndio kinara katika soko la dunia la zana zinazobebeka za nishati ya umeme na vifuasi vyake. Bosch huunda ubunifu katika zana za nguvu na vifuasi kwa kufanya kazi kwa bidii na wataalamu wanaotumia zana za nguvu kama sehemu ya kazi yao ya kila siku. 

Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni hiyo, Manoj Thakkar akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Upande wake Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni hiyo, Manoj Thakkar amesema kuwa kituo hicho kina zana za kisasa zaidi za nguvu za Bosch nakwamba wateja wataweza kujaribu bidhaa zao na kujionea ubora wa moja kwa moja.

“Aidha, tunashukuru kwamba kwa sasa mazingira ya biashara hapa nchini Tanzania yamekuwa rafiki ikilinganishwa na miaka ya nyuma, hili ni jambo linalotupatia msukumo wa kuendelea kutanua bidhaa zetu katika maeneo mbalimbali nchini, kupitia kituo hiki, NTS-Bosch kitahudumia na kuuza zana zote za umeme na vifaa vyake ,” amesema Thakkar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles