31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

NSSF YAWABANA WAAJIRI MICHANGO YA WAFANYAKAZI

NA CHRISTINA GAULUHANGA

-DAR ES SALAAM

WAAJIRI nchini wametakiwa kuhakikisha wanalipa malimbikizo ya michango ya wafanyakazi wao kabla ya Juni 30, mwaka huu ili kuepuka kufikishwa mahakamani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni, alisema waajiri watakaolipa malimbikizo yao ya michango ndani ya Mei na Juni mwaka huu watasamehewa tozo za malimbikizo kwa asilimia 100.

“Waajiri watakaolipa tozo (penati) za malimbikizo yao wanazodaiwa na shirika kwa asilimia  50 ndani ya kipindi hiki watasamehewa asilimia 50 ya tozo iliyobaki,” alisema Mmuni.

Alisema msamaha huo utaanza Mei 2, mwaka huu na kuishia Juni 30, mwaka huu.

Mmuni alisema fedha hizo zikipatikana zitasaidia kuendeleza miradi na kujenga viwanda.

Pia alisema wanatarajia kufunga mwaka wa fedha Juni mwaka huu hivyo ni vyema kila mwajiri akaleta malimbikizo yake.

Mmuni alisema wamepanga kukusanya kiasi cha Sh bilioni 23 kutoka kwa waaajiri  ambazo ni malimbikizo ya michango yao.

Aliongeza kuwa katika kuhakikisha oparesheni hiyo inafanikiwa wakaguzi watapita katika ofisi mbalimbali kuzungumza na waajiri ili malipo yafanyike kwa wakati.

Mwisho

Balozi Seif aongoza dua kuombea amani Z’bar

Na Othman Khamks Ame, OMPR

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, alisema mkusanyiko wa waumini wa dini ya kiislamu katika mfumo wa kushikamana bila ya kufarakana daima huzaa baraka zinazootesha neema na heri kwa umma na mbele ya Mwenyezi Mungu.

Kauli hiyo aliitoa juzi wakati wa dua maalumu ya kuliombea taifa amani na utulivu pamoja na kujiandaa kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuingia wiki chache zijazo.

Dua hiyo ilifanyika katika Msikiti wa Ijumaa Malindi mjini Unguja na kuhudhuriwa na mamia ya waumini wa dini ya Kiislamu na baadhi ya wiongozi wa Serikali.

Alisema waumini na wananchi wote wanapaswa kuzingatia  umuhimu wa suala la amani iliyopo nchini kwani kwa kufanya hivyo kutatoa fursa kwa waumini hao kutekeleza kwa utulivu ibada zao sambamba na kuendelea na harakati zao za maisha za kila siku.

Balozi Seif alitoa wito kwa wafanyabiashara wote kuacha tabia ya kupandisha bei za bidhaa muhimu zinazotumiwa kwa wingi na waumini wa dini ya kiislamu katika kipindi hicho cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Alisema tabia hiyo mbaya ni dhambi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitakuwa na huruma katika kuwachukulia hatua za kisheria wafanyabiashara  watakaopandisha bei za bidhaa bila sababu za msingi.

Mapema Mufti Mkuu wa Tanzania Bara,  Sheikh Abubakar  Zubeir Ali,  alisema dua ni fursa kubwa inayompa  mwanadamu kumuomba Mungu amwelekeze katika njia ya amani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles