25.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

NSSF, NBC kuendeleza uhusiano wa kibiashara

Mwandishi Wetu, Dar es SalaamShirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na  Benki ya NBC zimekubaliana kuendeleza na kukuza uhusiano wa kibiashara.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya uongozi wa Benki ya NBC kumtembelea na kufanya mazungumzo na  Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Septemba 21.

Erio aliishukuru benki hiyo kwa kuifanya NSSF kuwa mteja wake mkubwa zaidi katika huduma za kibenki na kuwa tayari kutoa ushauri wa kitaalamu utakaohitajika na shirika kwa sasa katika kuboresha huduma zao.

“Napenda kuwahakikishia kuwa ushirikiano uliopo utaendelea kuimarika chini ya uongozi wangu na kuhakikisha mifumo ya fedha za wananchama inaendelea kuwa salama na kutumika kwa maendeleo ya taifa,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Erio amesema ameishukuru NBC kwa kuendelea kutoa riba ya asilimia tano kwenye akaunti ya makusaanyo kutoka kwa wanachama wa NSSF.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi, amesema benki hiyo ni miongoni mwa taasisi ambayo serikali imeweka hisa zake na inajivunia kufanya kazi na NSSF, ambapo katika kuhakikisha wanahudumia wananchi kwa haraka NBC wana huduma za kibenki kupitia simu ya mkononi (mobile banking) inayoweza kuwafikia wananchi wengi waliopo vijijini wakiwamo wastaafu wa NSSF.

NBC imekuwa Benki ya nne kuweza kutembelea katika NSSF, tayari benki nyingine zikiwamo CRDB, NMB na UBA wameshakutana na NSSF na kupanga namna ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara baina yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,436FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles