NONDO ASHTAKIWA KUDANGANYA KUTEKWA, ANYIMWA DHAMANA

0
777

Na Francis Godwin, Iringa

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Iringa na kusomewa makosa mawili ya kutoa taarifa za uongo mitandaoni na kudanganya kutekwa.

Nondo amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano Machi 21, baada ya kusafirishwa usiku wa kuamkia leo akitokea Dar es Salaam alikokuwa akishikiliwa na polisi na kusomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali, Abel Mwandalama mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, John Mpitanjia.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Wakili wa Nondo Charles Luoga, alimuomba hakimu kumpatia dhamana mteja wake kwa kuwa makosa hayo yanadhaminika.

Hakimu alisema hawezi kumpa dhamana kwa sababu watekani bado wako mitaani na wanamshikilia kwa usalama wake ambapo aliahirisha shauri hilo hadi Jumatatu Machi 26, mwaka huu atakapojiridhisha sheria inasemaje

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here