27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

NMB YAZINDUA TAWI LA WATEJA MASHUHURI DODOMA

Na Mwandishi Wetu-DODOMA


BENKI ya NMB imezindua tawi la wateja mashuhuri wa Mkoa wa Dodoma na maeneo ya jirani kwa lengo la kuwahudumia wafanyabiashara wa maeneo hayo.

Akizungumza katika uzinduzi wa tawi hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker, alisema kuzinduliwa kwa tawi hilo la Makole Business Centre kunatokana na mji huo namna unavyovutia kwa wafanyabiashara na Serikali hasa kutokana na mpango wake wa kuhamia mkoani humo.

“Nia yetu ya kufungua Kituo cha Makole Business Centre ni kusisimua na kuona jinsi ya kuifungua Dodoma  hasa kutokana na maendeleo yaliyopo sasa. Ninayoyaona hapa ni tofauti na yale niliyoshuhudia katika ziara yangu mwishoni mwaka jana.

“Dodoma inaendelea kuwa muhimu kwetu kwa kuwa inaendelea kuvutia kila aina ya shughuli za Serikali na biashara. Na pia mpango wa Serikali kuhamisha ofisi za Serikali Dodoma. Pamoja na hoja hii, sisi changamoto yetu ni kuhakikisha kwamba tuna uwezo wa kutumikia mahitaji na kuongezeka kwa wateja na wafanyabiashara zaidi na watu binafsi hasa ya mkoa huu.

Alisea pamoja na hali hiyo, kihistoria benki hiyo imekuwa ikihudumia wafanyabiashara wadogo (SME) na tangu ilipobinafsishwa mwaka 2005, benki hiyo imekuwa na mafanikio lukuki na kuwa benki inayoongoza nchini.

Kwa upande wake mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jodan Rugimbana, alisema uzinduzi wa kituo cha biashara cha Makole utasaidia kusogeza huduma karibu na wateja hususani wafanyabiashara.

“Furaha yangu inatokana na ukweli kwamba huduma za kibenki ni kati ya huduma muhimu sana kwa ustawi wa jamii na maendeleo ya kiuchumi, kwa hili NMB mmekuwa wadau wakubwa wa kuchangia maendeleo ya kiuchumi nchini.

“Kama wote mnavyofahamu, Serikali ya awamu ya 5 ya raisi John Pombe Magufuli imeazimia kwa dhati kabisa kuhamishia shughuli zote za Serikali hapa Dodoma, kwa hiyo huduma za kibenki hasa kwa wafanyabiashara na watu mashuhuri ni muhimu sana,” alisema Rugimbana.

Alisema ufunguzi wa kituo hiki cha kibiashara cha Makole kitasaidia kuharakisha maendeleo ya wakazi wa eneo hilo na pia kurahisisha biashara zao kwa kuwasaidia kuokoa muda mwingi ambao wangeupoteza kwenda kupanga foleni kwenye matawi mengine ambako kila mtu anaenda kupata huduma.

“Nawapongeza NMB kwa kuona umuhimu wa kupanua na kuboresha huduma na sasa imetengeneza tawi maalumu la kuhudumia wateja wakubwa wenye mahitaji maalumu kama wafanyabiashara,” alisema. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles