25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 7, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yazindua tawi la huduma za benki inayotembea Dumila

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Benki ya NMB imezindua rasmi tawi la huduma za benki inayotembea katika mji mdogo wa Dumila wilaya ya Kilosa ikiwa ni mchakato kwa benki hiyo ya kujiandaa kwa ajili ya kujenga tawi kubwa kutokana na mji huo kuwa na majukumu ya kibiashara mkoani Morogoro.

Uzinduzi huo umeenda sambamba kwa benki hiyo kutoa msaada wa vifaa vya elimu kwa shule ya msingi Kilosa Town na shule ya sekondari Lumuma kwa viti na meza 50 na madawati 50 vyote vikiwa na thamani ya Sh milioni 10.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa benki ya NMB kanda ya kati, Nsolo Mlozi alisema wananchi wa Dumila waliokuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za kibenki ya benki hiyo sasa wataondokana na adha hiyo.

Mlozi alisema wakazi wa Dumila na vijiji vya jirani walikuwa wakipata shida kufikia na kupata huduma kutoka taasisi za kibenki.

“Sisi kama benki inayoongoza kwa faida nchini tumeonyesha mfano kwa kufungua tawi katika mji huo ili wananchi waweze kupata huduma mbalimbali za kibenki.

“Dumila ni mji wenye shughuli nyingi za kimaendeleo na wananchi wake wanaendesha shughuli nyingi za kiuchumi za kilimo, ufugaji, madini na kukosekana kwa taasisi ya kibenki ndio sababu iliyotupelekea sisi kuendelea kujitanua kwa kuzindua huu tawi la benki ya NMB,” amesema Mlozi.

Mlozi amesema benki hiyo imekuwa ikiisapoti serikali kwa wananchi kwa kutoa msaada kwa vifaa katika sekta ya elimu, afya, elimu ya utunzaji bora wa fedha na eneo la majanga ni sehemu wamekuwa kusaidia jamii wanaopata majanga.

Mkazi wa Dumila, Hawa Mohamed alisema sasa wananchi wa mji huo wataondokana na adha ya kutembea umbali mrefu waliokuwa wakifuata huduma za kibenki kutoka Dumila hadi Turiani kilometa 50, Dumila hadi Kilosa kilometa 60 na Dumila hadi Mvomero kilometa 20 ambapo kuna matawi ya benki hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Abdu Majid Mwanga alisema Dumila imekuwa na kilio cha muda mrefu wa uhitaji wa matawi ya mabenki na ufunguzi wa tawi la benki ya NMB inaenda kuondoa changamoto ya wananchi waliokuwa wakitembea umbali mrefu kwenda Kilosa, Turiani na Morogoro.

Mwanga alisema baadhi ya wananchi waliokuwa wakitunza fedha ndani ya nyumba wasiendelee tena kutunza fedha ndani wajitokeza kufungua akaunti katika benki hiyo ili kutunza fedha zao lakini kuchangamkia fursa zinazotolewa na benki ikiwemo mikopo ya fedha yenye riba nafuu.

“Siwapigii debe hawa NMB kwani wamekuwa na mikopo ya wafugaji ili kufuga kwa kisasa lakini ipo ya kilimo na mikopo ya pikipiki za matairi mawili na matatu mchangamkie hizi fursa na wilaya tunawashukuru kwa misaada ya vifaa mbalimbali katika sekta ya elimu, afya na pale majanga yanapojitokeza tumekuwa tukinufaika nao,”amesema Mwanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles