22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yazindua hati ya kiapo cha huduma kwa mteja

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Benki ya NMB jana ilizindua maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja kwa kuahidi kuwahudumia kwa viwango bora vya hali ya juu ili kuendelea kuwa taasisi ya fedha pendwa na inayoongoza nchini.

Ahadi hiyo ipo kwenye Hati ya Kiapo cha Huduma kwa Mteja ambayo benki hiyo iliizindua samabamba na uzinduzi wa shughuli za wiki ya wateja ambazo kitaifa ilifanya jijini Dodoma.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Ruth Zaipuna (Wa Pili Kushoto) akimkabidhi Hati ya Kiapo cha Huduma kwa Wateja Mkuu wa Mkoa wa Dodoma – Anthony Mtaka (wa Tatu Kushoto) muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi wa hati hiyo uliofanyika jijini Dodoma jana ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa wateja. Wengine ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini – Anthon Mavunde ( wa Kwanza kushoto), Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara – Filbert Mponzi (Mwanzo Kulia), Mkuu wa wilaya ya Bahi -Mwanahamisi Mukunda (Wa Pili Kulia), Mbunge wa Jimbo la Bahi – Keneth Nolo (Wa tatu Kutoka Kulia).

Katika hafla hiyo na kama sehemu ya sherehe za kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, NMB pia ilitoa misaada mbambali mkoani huo yenye thamani ya Sh 40 milioni yakiwemo madawati na vifaa vya hospitali.

Shughuli kama hizo zilifanyika katika kanda zote za benki hiyo nchini zikiongozwa na viongozi wa ngazi za juu ambako pia misaada mbalimbali ilitolewa.

Ngeni rasmi jijini Dodoma, ambako Afisa Mtendaji Kuu wa NMB, Ruth Zaipuna, alisema hati hiyo ni maazimio na matamanio ambayo NMB imejiwekea ili kufikia adhma ya kutoa huduma bora, shindani na yenye tija, alikuwa Mkuu wa Mkoa, Anthony Mtaka.

Tukio hilo pia lilihudhuriwa na wabunge wa Mkoa wa Dodoma, wakuu wa wilaya watatu za mkoa wa Dodoma, wateja wa NMB na viongozi mbalimbali walioipongeza benki hiyo kwa ubunifu na ubora wa huduma zake huku wakisema uwekezaji inayoufanya katika maendekleo ya taifa ni mkubwa na wa kuigwa.

Zaipuna alisema Hati ya Kiapo cha Huduma kwa Mteja ni nyenzo muhimu katika kuweka uhusiano mzuri na wateja wa benki hiyo ili waendelee kuiamini na iweze kuendeleza ushindani wenye tija sokoni. Mkataba huo wa hiari pia unaiwezesha NMB kuweka maazimio ya uhusiano wa kibiashara wenye afya na wateja wake.

“Leo tunaungana na dunia nzima kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, inayoadhimishwa kila mwaka wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba,” Zaipuna alisema kabla ya kutangaza rasmi kuzindiliwa kwa hati hiyo ya kiapo.

“Kauli mbiu ya Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa mwaka huu ni ‘Nguvu ya Huduma’ na ili NMB iendelee kuongoza kwenye utoaji huduma kwa wateja, maadhimisho haya tunayatumia kuzindua Hati ya Kiapo cha Huduma kwa Mteja kuonyesha kwa vitendo nguvu ya huduma kwa wateja wetu,” kiongozi huyo alifafanua.

Wiki ya Huduma kwa Wateja ni maadhimisho ya kimataifa ya umuhimu wa huduma kwa wateja na ya watu ambao wanahudumia na kusaidia wateja kila siku. 

Katika kulitambua hilo, NMB jana iliwatunuku vyeti maalum wateja na wafanyakazi wake ambao ndiyo wachagiaji wakubwa wa mafanikio yake. Kupitia, hati hiyo ya kiapo, watumishi wa NMB wanajua nini kinategemewa kutoka kwa wakati wa kutoa huduma na wateja nao wanapata haki ya kujua nini watarajie kutok benki hiyo.

Zaipuna alisema kimsingi hati hiyo ina ahadi tano za benki kwa mteja ambazo ni kupatikana kwake kwa haraka, usikivu, uhakika na kuaminika, usalama wa taarifa za mteja pamoja na weledi na nidhamu. 

Akiwapongeza wateja kwa kuiunga mkono benki hiyo na kuchangia mafanikio yake, Zaipuna alifafanua kuwa ahadi hizo ni maazimio yatakayolinda haki ya mteja na pia yenye kudhamiria kudumisha uhusiano wao mzuri.

“Mbali na wateja, naomba pia niwashukuru wafanyakazi wenzangu wa Benki ya NMB kwa kazi kubwa wanayofanya, benki hii imekuwa ikiongoza kwa kila kitu sababu ya utendaji mzuri na uaminifu wao, na ndiyo nguzo tunayosimamia,” alisisitiza.

Mtaka aliitaka NMB kutochoka na ukarimu wake ambao hata viongozi wengine walisema umekuwa ni chachu kubwa ya kuyabadilisha maisha si tu ya wakazi wa Dodoma bali pia Tanzania nzima.

“Suluhishi zenu bunifu za kifedha na uwekezaji mkubwa mnaoendelea kuufanya ni vitu vinavyoifanya NMB kuwa benki kubwa na kiongozi wa maendeleo nchjini,” Mw Mtaka alisema.

Misaada mabayo NMB iliitoa jana Dodoma ni pamoja na vifaa vya hospitali kwa ajili ya Hospitali Wilaya ya Bahi na Zahanati ya Chimedeli. Pia vimo viti 200 na meza 200 kwa ajili ya shule za sekodari Nondwa, Msisi Juu, Sechelela na Ibihwa pamoja na madawati 50 kwa ajili ya Shule ya Msingi Chiguluka na mabati kwa ajili ya Shule ya Sekondari Bahi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles