25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yawakutanisha Wafanyabiashara mikoa ya Dodoma, Singida

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Benki ya NMB jana imewakutanisha wafanyabiashara wakubwa na wadogo wa mikoa ya Dodoma na Singida katika usiku wa Mtandao thabiti kwa ukuaji endelevu wa Biashara.

NMB kupitia  ‘Business Executive Network’  (BEN) na ‘Business Club’ wamejumuisha  wafanyabiashara zaidi ya 700  kutoka Mkoa wa Singida na Babati (Manyara) kwa nyakati tofauti.

Mkuu wa  kitengo cha biashara benki ya NMB (Head of Business Banking) , Alex Mgeni  akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa  Mikoa ya Kanda ya Kati ,Dodoma na Singida walipokutana  jana usiku Jijini Dodoma. NMB iliandaa na kukutana na wafanyabiashara zaidi 600 kwa ajili ya kutoa elimu ya kifedha, kodi na  huduma zinazotolea na benki hiyo. 

Katika usiku wa pamoja NMB walitoa mafunzo ya uendeshaji wa biashara na mikopo huku wakitangaza kiwango kikubwa cha mteja mmoja kuruhusiwa kukopa ni hadi Sh250 bilioni kutegemea na uwezo wake.

Meneja Mwandamizi wa NMB kitengo cha biashara Christopher Mgani alisema kutokana na kukua kwa mtaji ndani ya NMB, sasa wanaweza kutoa kiasi kikubwa na kwa marejesho ya muda mrefu kwa wateja wao.

Taarifa zinaeleza kuwa benki hiyo imefikia mtaji wa zaidi ya Sh7 trilioni huku ikiwa imeongoza kwa miaka nane mfululizo kuwa benki bora nchini.

Mgani alisema wameendelea kuboresha mikopo na Mazingira ya ukopeshaji ambayo yamekuwa rafiki mkubwa kwa wafanyabiashara wa aina zote nchini huku wakisogeza karibu huduma za fedha kupitia NMB mkononi na Wakala zaidi ya elfu 9,000 nchi nzima.

Kingine alifafanua kuhusu mikopo ya kujenga, kumalizia au kununua nyumba ambayo alisema ni rafiki kwa kila mtu kulingana na kiwango cha mtaji wake na marejesho yake yanakwenda hadi miaka 15.

Mkuu wa kitengo cha biashara makao makuu Alex Mgeni alisema maboresho makubwa yamefanyika ndani ya benki na yote yakilenga kutoa unafuu kwa wateja wao kwa kuwa NMB ndiyo kimbilio la wote.
Mgeni alisema wamefungua milango ya majadiliano na wateja wao siku 30 kabla ya kufanya marejesho pindi wanapohisi wamekwama na benki inafanya ufuatiliaji ili kuwasaidia kujikwamua.

“Kipaumbele chetu ni kuona wateja hawapati misukosuko katika biashara zao hasa kwenye marejesho kwani kukwama kwao ni kukwama kwa benki na sisi watumishi jambo ambalo hatukubali,” alisema Mgeni.

Mmoja wa wateja wa NMB Neema Mandala alisema katika maisha yake ya biashara anajivunia kuwa na benki hiyo kutokana na kupatiwa miongozo na maelezo ya watumishi.

Neema aliomba benki kuendelea kupanua wigo wa kuwafikia wahitaji wengi zaidi katika mpango wa kuwaleta pamoja kwani wanapata fursa ya kubadilishana uzoefu wa biashara.

Hata hivyo alisisitiza kwa wafanyabiashara na Watanzania wengine kutumia NMB kwa ajili ya kukuza uchumi wao kwa na kuongeza mitaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles