23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yawahimiza Walimu kuwekeza na kuchangamkia mikopo nafuu

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Walimu wametakiwa kuwekeza na kujiendeleza katika kukopa mikopo nafuu yenye tija yakuweza kutatua  changamoto zinazowakabili ili kuweza kunufaika na kufurahia kazi wanayoifanya.

Washiriki wa Semina ya walimu wakuu wa Shule za msingi na Sekondari zilizopo Mkoa wa Arusha,wakisikiliza Hutuba ya mgeni rasimi,kwenye uzinduzi wa semina ya  mafunzo ya bidha za NMB. Semina hiyo yenye lengo lakutoa elimu ya fedha na bidhaa mbalimbali za NMB ilifanyika jana katika Ukumbi wa Rashi Garden Arusha mjini nakuhudhuriwa na walimu zaidi 300.

Akizungumza Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongella katika mafunzo ya walimu wa mkoani hapo  yaliyoandaliwa na Benki ya NMB ambaye ni Afisa elimu sekondari, Khalifani Omary alisema mafunzo hayo yatawajenga walimu katika kujiwekea kipato ili kuweza kujiendeleza kimaisha.

“Mafunzo haya yatawasaidia katika kuwaongezea elimu na kutoa fursa ya maoni namna wanavyoweza kunufaika na benki ya NMB ikiwa jitihada hizi zitaleta matokeo chanya nakuleta faraja kwa jamii,”alisema Omary.

Afisa elimu alisema jitihada hizo ni nzuri na  zinaunga mkono juhudi za serikali katika kuhakikisha watanzania waliowengi wanajumuhishwa katika mfumo rasmi wa kifedha ili kuinua  vipato vyao na kiuchumi kwa ujumla hivyo anatoa rahi kwa taasisi nyingine za kifedha nchini kufanya jitihada hizo kama NMB.
Alisema anashukuru huduma za kibenki zimeboreshwa na kusogezwa karibu na wateja wake kwani hapo awali walimu walipata taabu kutembea umbali mrefu hivyo benki ya NMB imekuwa chachu ya maendeleo katika jamii kwa kuwanufaika wateja wake.

Kwa upande wake Mkuu wa biashara za Kadi wa benki ya NMB, Philbert Casmir  alisema  wameandaa mafunzo yanayoitwa siku ya walimu ambapo wameanza mkoani Arusha kwa kutambua mchango wa mwalimu katika jamii na kutoa suluhisho ya changamoto zao katika kujikwamua kimaisha ikiwemo mikopo nafuu na bima mbalimbali.

“Tunatambua mwalimu ni mwezeshaji  katika jamii hivyo NMB tumekuja na muundo wa kutokutoa bidhaa au suluhisho ya maisha ya walimu kwani tunatambua kunachangamoto za ujenzi na kupitia mafunzo haya wataelimishwa nakuweza kutumia mikopo nafuu ya NMB kujiendeleza katika swala la ujenzi wa nyumba,”alisema Mkuu huyo.

Meneja wa  wateja binafsi Benki ya NMB (Manager Personal Banking), Nyamisinda Manyonyi akitoa elimu ya Mikopo kwa walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari Mkoa wa Arusha. Semina hiyo yenye lengo lakutoa elimu ya fedha na bidhaa mbalimbali za NMB ilifanyika jana katika Ukumbi wa Rashi Garden Arusha mjini.

Casmir alisema pia kuna bima za walimu na watanzania kwa ujumla zinazoweza kuwasaidia kupata fedha pamoja na hilo pia kunachangamoto ya elimu ya fedha watu kutoweka fedha katika taasisi za kibenki na kutunza majumbani hivyo elimu hiyo itawasaidia kufikisha ujumbe na faida za   kuweka fedha benki katika jamii.

Baadhi ya walimu hao walisema wanashukuru benki ya NMB kwa kuwapa mafunzo hayo ambayo yatawasaidia katika kuwekeza fedha nakutumia katika matumizi sahihi ya kujiendeleza kiuchumi na kuwaletea maendeleo katika jamii.

Mwalimu  mkuu wa shule ya msingi Daraja mbili , Zukra Kalunde alisema mafunzo hayo yatawasaidia katika kufahamu umuhimu wa kadi pamoja na kujifunza namna ya kupata mikopo nafuu ya benki hiyo itakayowasadia kujiendeleza kiuchumi kama ujenzi wa nyumba zao za kuishi na biashara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles