31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yatoa mabati kwa shule Serengeti

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Katika kuthibitisha uwajibikaji wao kwa jamii, Benki ya NMB imetoa wa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 8 katika shule ya msingi Bwitengi iliyopo katika kijiji cha Bwitengi kata ya Manchira wilaya ya Serengeti mkoani Mara.

Akizungumza katika hafla fupi ya makabadhiano iliofanyika leo katika shule ya msingi Bwitengi, Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Ziwa, Baraka Ladislaus amesema wataendelea kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Serengeti katika shughuli za maendeleo.

“Tulipopata maombi kutoka shule hii, sisi kama NMB tukaona ni vyema tukawasaidia na leo tumeweza kuwaletea Mabati 118,Mbao 400,Kilogramu 80 ya Misumari na waya za kushikia kenchi Kilogramu 16” amesema Ladislaus. Benki yetu itaendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya rais wetu, Mama Samia Suluhu Hassan,” ameongeza.

“Benki yetu itaendelea kuinua sekta ya elimu na kwa mwaka huu, tutaanza ufadhili kwa wanafunzi wanaotakiwa kujiunga na chuo kikuu lakini wakishindwa kwa sababu za kiuchumi. Benki ya NMB itawagharamia ada malazi pamoja na kuwapa vitendea kazi kama compyuta kuwasaidia masomoni,” amesema.

Aidha, Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Dk. Vicent Mashinji ameipongeza benki ya NMB kwa kutoa msaada wa vifaa vya ujenzi. Amewaomba wakazi wa kijiji cha Bwitengi na wanaserengeti kwa ujumla kuendelea kushirikiana vyema na Benki ya NMB klwani ndie mshirika wakweli kwa maendeleo ya wilaya ya Serengeti. 

Mkuu wa shule ya msingi Bwitengi, Melau Mollel alisema anaishukuru sana benki ya NMB kwa kuisaidia shule yao. Huku akiwaomba wasichokee kuisaidia shule yao kwani bado wan mahitaji mengi ikiwemo mashimo 32 ya vyoo ili kukidhi idadi kubwa ya wanafunzi waliyo nayo.

Alisema wanakabiliwa na uhaba wa nyumba 18 za walimu,ofisi Tatu za walimu na madawati 266. Ameomba kusaidiwa upatikanaji wa photocopy mashine mbili pamoja na matanki manne ya maji. Mollel alisema bado kuna ushiriki mdogo sana wa wazazi katika kusimamia Elimu kwa watoto wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles