31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 5, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yatoa hisani ya mabati, vifaa maabara shuleni

Shermarx Ngahemera

BENKI ya NMB inasema ina mabadiliko makubwa katikakushughulikia Hisani kwa Umma (CSR), ambapo malengo yake sasa ni kufadhi limiradi ya mendeleo ya elimu na afya kutokana na sera ya Serikali ya elimu bure kuonekana kuongeza mahitaji makubwa ya vyumba vya madarasa na vyumba vya maabara kutokana na kuongezeka idadi ya wanafunzi.

Benki hiyo inasema mwitikio kutoka kwa umma umekuwa mkubwa sana ambapo zaidi ya maombi 15 hupokelewa kila siku yakidai kupatiwa msaada juu ya mahitaji ya shule  mbalimbali  nchini kutokana na kuwa ina matawi katikawilaya zote nchini na hivyo, ni shughuli nzito kufanya udhibiti wa mahitajihayo na mwishowe kufanya malipo au kutoa vifaa vya ujenzi kukamilisha majengohayo.

Ofisa Uhusiano na Umma akiongea kwa sharti la kutotajwa jina kwani sio ofisa stahiki kutoa maelezo hayo amesema kuwa hadi sasa zimeshalipwa, au kutoa mali ya thamani ya jumla ya shilingi zaidi ya bilioni moja kwa shule mbalimbali nchi nzima.

Anasema ufadhili huo hutolewa baada ya maombikuwafikia wao na kwenda kukagua majengo husika na wakisharidhika kuwa ujenzi umekuwa sawa na kusubiri paa tu ndipo huwa rahisi kufadhili mabati ya kuezekea ili kukamilisha ujenzi husika.

Kwenye maabara, vyumba vinatakiwa kuwa tayari vimejengwa na wao benki hugharamia  upatikanajivifaa, samani za  maabara na madawahusika ya kuanzia shughuli za kufanyia majaribio kwa vitendo kwa masomombalimbali.

Afisa huyo anasema inatia moyo kuona wazazi wenyewe kutoka kila pembe ya nchi wakichanganyishana fedha ili kuboresha  elimu ya vijana wao.

Tanzania ina mpango kabambe wa kuwa nchi ya uchumi wa viwanda na kutegemea kufikia kiwango cha kuwa nchi ya uchumi wa kati mnamo mwaka 2025 na kufikia malengo haya inabidi juhudi ifanyike kwenye masomo ya sayansi na teknolojia.

Benki hiyo imejizatiti vilevle kwenye kutoa madawati hadi 200 kwa kila shule inayooomba ili kuwe na hali murua ya kusoma kwa wanafunzi  husika katika shule wanazotoa misaada husika na hivyo kuwezesha taifa kupata wataalamu wa kesho ili nchi iweze kufanya mapinduzi ya kimaisha kwa kuwa na mazingira mazuri ya kusomea.

Uhisani wa benki hiyo unatokana na ukweli wa kuwa na mahusiano mazuri na serikali kwani ni benki teule kwake kwa kutoa huduma mbalimbali za kibenki na vilevile ni mwanahisa wa benki hiyo inayoongoza kwa ukubwa wa mali (assets) nchini.

Benki NMB ina matawi kila wilaya na ATM zaidi ya 700 nchini kote  na utititiri wa mawakala (agency banking) na imepiga hatua kubwa kwa utoaji wa huduma za kibenki kidijitali kwa Klik au kadi ya benki kwa kupangusa na au QR Codes unafanya  scan.

Benki inajitahidi kuwa na jamii isiyotumia sanafedha taslimu hadi kuwa ‘cashless society’ nchini ili kuzilinda fedha dhidi yakupotea kwa wizi au kwa gharama mbalimbali zilizofichika na kwenye upelekajimiamala mbalimbali. Benki ya NMB huduma zake sio ghali  kama zile za kutumia miamala ya simu.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                     

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles