24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yakabidhi vifaa vya huduma ya Afya Kongwa

Mwandishi Wetu, Korogwe

Benki ya NMB imeahidi kuwa itaendelea kuunga mkono juhudi za wananchi katika mipango ya maendeleo ikiwemo Sekta za afya na Elimu ambazo zinagusa jamii moja kwa moja.

Ahadi hiyo ilitolewa Septemba 18, na Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi wakati akikabidhi vifaa vya huduma za afya kwa uongozi wa wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma katika Kongamano la maendeleo la wilaya ambalo lilihusisha watu wengi katika ukumbi wa VETA mjini hapa.

Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi (watatu toka kushoto ) akiiwa na  Mkuu wa Wilaya ya Kongwa ,Remidius Emmanuel (kulia) pamoja na  Spika wa Bunge ,Job Ndugai na  pili kulia Spika wa Bunge mstaafu, Anna Makinda, mwisho kushoto  Kaimu meneja wa NMB Tawi la Kongwa, Christina Niniko na wapili kushoto ni Meneja Mahusiano NMB na  Serikali Kanda ya Kati ,Peter Masawe, wakishangilia mara baada ya makabidhiano ya vifaa tiba vyenye  thamani ya sh milioni 10 kukabidhiwa jana kwa ajili ya vituo vya afya vya Hogoro na Sejeli vyote vya Wilayani hapo Mkoani Dodoma.

Mlozi alikabidhi mashuka, vitanda na baadhi ya vifaa kwa ajili ya akinamama kujifungulia vikiwa na thamani ya Sh milioni 10 na vililwnga zahanati za Hogoro na Sejeli zilizotajwa kuwa na upungufu.

Kwa mujibu wa NMB, mwaka huu benki hiyo imeshatoa msaada wa vitu vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 40 kwa wilaya ya Kongwa ikiwa ni sehemu ya asilimia moja ya faida yake ambayo hurudishwa kwa wananchi.

“Mbali na hivyo vifaa lakini tumesaidia kuandaa Kongamano hili la maendeleo na niseme kwa niaba ya uongozi wa NMB tutaendelea kusaidia katika shughuli za kijamii ambazo ni elimu,afya na Elimu ya utunzaji wa fedha kwa vijana, benki hii ni yenu endeleeni kuitumia,”alisema Nsolo.

Alisema msaada huo ni sehemu ya faida baada ya kodi ambayo NMB ilipata msimu uliopita iliyokuwa Sh206 bilioni na asilimia moja inayorudi kwa jamii ni Sh2.6 bilioni ndizo hutumika kusaidia katika huduma za kijamii.

Mkuu wa wilaya ya Kongwa Remigius Emmanuel alisema msaada wa NMB ni muhimu kwa ajili ya kusaidia jamii ya watu wa kada za chini na ndiyo maana wameendelea kuona benki hiyo ni ndugu yao.

Emmanuel alisema wataendelea kushirikiana na NMB kwa mambo mengi kwa kuwa imejipambanua kuwa ipo kwa ajili ya watu hivyo wameona mashirikiano kwa mambo mengi ya kimaendeleo yatadumishwa.

Kuhusu Kongamano hilo alisema liliandaliwa na Ofisi yake Kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo benki hiyo ambayo mbali na kusaidia fedha lakini walitoa utaalamu wa namna gani ifanyike.

Mkazi wa Sejeli Mwajuma Mwaluko alisema vifaa vilivyotolewa vitakuwa mkombozi hasa kwa akina mama na watoto kwa kuwa ndiyo wahanga wakubwa kwenye masuala ya afya.

Mwajuma aliomba wadau wengine kuunga mkono juhudi za NMB katika kuboresha huduma za afya Vijijini kwani hali bado si nzuri licha ya juhudi za Serikali na wananchi lakini ongezeko la watu linapelekea kuwe na mapungufu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles