31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yakabidhi madawati ya Mkuranga

NA MWANDISHI WETU

BENKI ya NMB imetoa msaada wa viti 50, meza 50 na madawati 62 vyenye thamani ya sh. 10 milioni kwa Shule ya Sekondari Mkugilo na Shule ya Msingi Chatembo, wilayani Mkuranga, Pwani, kiasi kinachoifanya benki hiyo kufikisha zaidi ya sh. bilioni 1.8 zilizosaidia sekta za Elimu na Afya tangu  Januari 2021.

Msaada huo, umetolewa katika hafla iliyofanyika viwanja vya shule ya sekondari Mkugilo ambapo Meneja Mahusiano, Biashara za Serikali wa NMB Kanda ya Mashabiki, Aneth Kwayu, alimwakilisha meneja wa kanda hiyo, Dismas Prosper na kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Khadija Ally.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na Mkurugenzi wa Wilaya ya Mkuranga, Mshamu Munde, Kwayu amesema mgawanyo wa msaada huo ni viti 50 na meza 50 kwa ajili ya sekondari ya Mkugilo, huku madawati 62 yakienda shule ya msingi Chatembo na kwamba urejeshaji kwa jamii ni sehemu ya utamaduni wa muda mrefu wa NMB.

Kwayu amebainisha kuwa, Programu ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), inatumia asilimia moja ya faida ya benki yake kwa mwaka uliotangulia kusaidia nyanja za elimu, afya na majanga,tangu Januari mwaka huu, NMB imetumia zaidi ya sh. Bilioni 1 na milioni 88, kati ya sh. Bilioni 2 ilizotenga na kupanga kuzitumia mwaka huu.

Kupitia hotuba yake kabla ya kukabidhi msaada huo, Kwayu amesema NMB inazitazama changamoto za sekta ya elimu kama moja ya vipaumbele vyake vikuu, kutokana na ukweli kuwa elimu ndio ufunguo wa maendeleo sio tu ya mtu mmoja mmoja, bali  kwa Taifa.

“Tunatambua jitihada za Serikali ya Rais Samia Suluhu, iliyojikita katika kuboresha mazingira ya utoaji elimu bure mijini na vijijini na kimsingi tunaipongeza, nasi tukiwa wadau vinara wa sekta hiyo tunajiona tunao wajibu wa kuunga mkono juhudi zozote za kusaidia jamii, ambayo ndio imeifanya NMB kuwa hapa ilipo.

“Tunawashukuru viongozi wa shule mbalimbali nchini wanavyoichagua NMB wanapokuwa na uhitaji, hii inaonesha kuwa mnathamini mchango wetu kwa maendeleo ya jamii na sisi tunafurahia kujitoa kwetu na tutahakikishia jamii inayotuzunguka inanufaika na faida tuipatayo,” amesema Kwayu.

Akizungumza wakati akipokea msaada huo, DC Khadija aliimwagia sifa NMB kwa namna ilivyojipambanua katika usaidizi na utatuzi wa changamoto za sekta ya elimu na afya nchini, na kwamba yeye sio tu balozi mwema, bali ni shuhuda wa harakati chanya za benki hiyo katika kunyanyua elimu kote nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles