24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

NMB yakabidhi gari kwa mkazi wa Chamwino kupitia kampeni ya Bonge la Mpango

Mwandishi Wetu, Dodoma

Gari laa kwanza katika Kampeni ya Bonge la Mpango inayoendeshwa na benki ya  NMB, jana ilikabidhiwa kwa Hadija Iddi mkazi wa Chamwino Ikulu mkoani Dodoma.

 Hadija anakuwa mshindi wa kwanza katika zawadi kubwa zinazotolewa na NMB katika Kampeni iliyoanza mwezi Februari mwaka huu.Akikabidhi gari hiyo aina ya Tata Ace almaatufuu kama Kirikuu na yenye thamani ya milioni 25 jana, Kaimu Afisa Mkuu Ukaguzi wa ndani kwa NMB, Benedicto Baragomwa alisema kampeni hiyo inaendelea nchini kote na zawadi mbakimbali zinaendelea kutolewa.

Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Benki ya NMB ,Benedicto Baragomwa (Ag.Chief Internal Audit) akimkabidhi gari ,Jacqline Kihongozi, aliyepokea kwa niaba ya Mshindi la kampeni ya bonge la Mpango inayoendeshwa na Nmb ,Hadija Idd Mkazi wa Chamwino Ikulu, Mkoani Dodoma jana ,mshindi huyo amekuwa ni mshindi wa kwanza kujishindia zawadi ya gari aina ya Tata Ace kwenye kampeni hiyo.

Baragomwa alisema NMB inatoa zawadi kwa wateja  wanaendelea kufungua akaunti zao na kuwa mshindi wa jumla atajinyakulia gari ya kifahari. Gari itakayotolewa ni Toyota Fortuner yenye thamani ya Sh ilionni 169 ambayo zero kilomita.

“Ndugu Watanzania, hapa namkabidhi Hadija ufunguo wa gari yake kama mnavyoona ni jipya, lakini tunazo zawadi nyingi kwa wateja wetu wanaoweka akiba kuanzia Sh 100,000 kwenye akaunti zao za NMB,” alisema Baragomwa.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa gari yake, Hadija alisema hajuamini kilichotokea na kuwa hakuwa amepanga lakini no mpango wa Mungu.

Hadija alisema gari hiyo TATA Ace yenye thamani ya Sh25 milioni itamsaidia katika shughuli zake za kujiongezea kipato lakini akawashauri Watanzania kuwekeza katika benki hiyo kwa kuwa ina manufaa makubwa.

“Nimeamini kuwa yanayozungumzwa ni kweli,nimekabidhiwa gari mpya,nimepewa ufunguo na Kadi ya gari vikiwa kamili kabisa, kweli NMB ndiyo mpango mzima,”alisema Hadija.

Wakati huo huo Meneja wa NMB kanda ya Kati Nsolo Mulozi aliongoza droo nyingine kwa ajili ya ya washindi ambapo watu mbalimbali walipata fedha baada ya kushinda.

Droo hiyo ilifanyikia katika benki hiyo Tawi la Chamwino Ikulu chini ya usimamizi wa viongozi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha.

Hadi jana, NMB ilikuwa imetoa zawadi zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 145 zikiwemo fedha taslimu, pikipiki za miguu mitatu aina ya LIFAN 16 na gari iliyotolewa jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,220FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles