28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

NMB Watoa gawio, Dk. Mpango akifurahi

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Benki ya NMB imetoa gawio la Sh bilioni 21.8 ikiwa ni ongezeko la asilimia 43 ya gawio la mwaka jana ambalo  lilikuwa Sh bilioni 15.25..

Akipokea mfano wa hundi leo Ijumaa Juni 18, 2021 jijini Dodoma, Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango amesema kiasi hicho kimemridhisha kwa mwaka huu lakini akataka waongeze maarifa zaidi ili kutoa gawio la juu ikiwemo kuwekeza katika nchi majirani.

Dk Mpango amesema kiwango kilichotolewa mwaka jana hakikumfurahisha ndiyo maana akaagiza lazima waongeze juhudi lakini kwa mwaka huu amebarikiwa.

Gawio lililotolewa leo ni sehemu ya faida ya Sh bilioni 206 ambazo benki hiyo ilipata katika msimu wa kuishia Desemba 2020 baada ya kuondoka kodi.

Serikali inapokea gawio hilo kutokana na umiliki wake wa hisa asilimia 31.8 ndani ya benki hiyo ambayo kwa miaka 8 mfululizo imekuwa ikipata tuzo ya benki bora nchini.

“Nimefurahishwa sana na hiki mlichotoa, pamoja na mafanikio haya lakini nataka muongeze ubunifu ili mwaka muwe zaidi ya  hapa, hata hivyo nakuagiza Waziri wa Fedha kwamba kiasi hiki kikafanye kazi nzuri kwa wananchi ambayo imekusudiwa,” amesema Dk Mpango.

Kuhusu NMB aliwataka kushirikiana na Taasisi zingine ili wakae na benki Kuu (BoT) kujadili kuhusu riba kubwa ambayo bado inatozwa na mabenki na hivyo kusababisha watu washindwe kukopa.

Amewataka viongozi wa taasisi ambazo Serikali ina hisa lakini hawatoi gawio kwamba wajitathimini vinginevyo watachunguzwa na watakaokuwa wamekiuka kanuni Serikali itawapeleka Segerea hata kama kumejaa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Edwin Mhede amesema tayari fedha hizo zilishawekwa katika akaunti ya msajili wa Hazina na kwamba mwakani watakuwa na kiasi kikubwa zaidi kutokana na mwenendo wavyoona.

Mhede ametaja siri kubwa ya mafanikio ya NMB ni ubunifu na kutljituma kwa watumishi wao katika kuutafuta masoko lakini utoaji bora wa huduma unaowabutia watu kuitumia benki hiyo.

Mtendaji Mkuu wa NMB Ruth Zaipuna alisema mbali na gawio hilo,lakini wamelipa serikalini Sh bilioni 245 kama kodi za tozo mbalimbali na kutumia asilimia moja ambayo ni zaidi ya Sh bilioni 2 kwenye huduma za kijamii.

Zaipuna alisema benki hiyo imefikia mtaji was Sh trilioni 1.1 kutoka Sh660 bilioni kwa mwaka 2015 hivyo ukuaji wake unatia matumaini kwamba itaendelea kuwa ni benki bora yenye kutoa huduma kwa viwango vinavyotakiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles