30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

NMB kunogesha mbio za Zanzibar International Marathon Julai 18

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Benki ya NMB (NMB Bank Plc) imedhamini mbio za KM 5 za Zanzibar International Marathon 2021 zinazotarajiwa kufanyika 18 Julai mwaka huu zenye lengo la kukuza Utalii na Uchimi wa bluu Zanzibar.

Akizungumza wakati wa uzinduzi mdogo wa utambulisho wa mbio hizo kwa upande wa Tanzania Bara, ulifanyika ndani ya duka la Just Fit Sports Gear Mlimani City, Meneja wa Biashara za NMB Zanzibar, Abdalla Duchi alisema wameunga mkono harakati za Serikali kuiona Zanzibar inakuwa kiuchumi haswa uchumi wa bluu.

“NMB Zanzibar tunaendelea kutoa huduma bora za kibenki ambapo ni moja ya fursa za kukuza uchumi.
Naomba tuendelee kujiandikisha kushiriki mbio hizi ili kutangaza Utalii na pia kuimarisha afya.” Alisema Duchi.

Aidha, Duchi aliweka wazi kuwa, NMB imedhamini mbio za KM 5 ambazo tayari pia viongozi wakuu wa nchi wamethibitisha kushiriki.

“Kupitia mbio za NMB KM 5 za Zanzibar International Marathon tayari Rais Dkt. Hussein Mwinyi wakiwemo Makamu wake wa kwanza na wa Pili wa Rais na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wamethibitisha kukimbia mbio hizo,” Alisema Duchi.

Nahodha wa NMB Jogging Club Jessica Sanga, alisema wapo katika mazoezi ya kushiriki mbio hiyo Julai 18 mwaka huu na wataendelea kuhamasisha wengine.

“NMB Jogging Club tupo wanachama zaidi ya 100 na wote wamekubali kushiriki kwenda Zanzibar International Marathon”. Alisema Jessica.

Katika tukio hilo pia viongozi mbalimbali wa Serikali wa Zanzibar na Tanzania Bara walishiriki wakiwemo Katibu wa Wizara ya Habari Zanzibar, Khamis Said, Katibu Mkuu Utalii Zanzibar, Fatma Mbarouk Khamis aliyemwakilisha Waziri wa Utalii Zanzibar.

Kwa upande wao kampumi ya Vodacom kupitia kwa Afisa Masoko na Mawasiliano, Kitengo cha Lipa Kwa Simu (Vodacom), Bw. Mario Mpingirwa alisema wametoa punguzo la asimia 10 kwa wateja watakaolipa kwa simu.

Mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika 18 Julai mwaka huu kila mshindi ataibuka na zawadi nono:
Zawadi hizo ni pamoja na: Milioni 3,000,000 kwa washindi wa KM21 kike/kiume, Mil 2,500,000 kwa washindi wa pili na Sh milioni 1,000,000 kwa mshindi wa Tatu huku washindi wengine hadi 10 wataibuka na Tsh Laki moja kila mmoja.

Kwa mbio za KM 10, Mshindi wa kwanza ni Mil 2,500,000, Mshindi wa wa pili 2 ni Mil 1,000,000 na wa Tatu ni Sh 750,000.

Mbio za KM 5 mshindi wa kwanza ni mil 1,000,000, wa pili Sh 750,000 na wa Tatu ni Sh 500,000.
Aidha, kwa upande wa Walemavu watatoa zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu pekee ikiwemo Mshindi wa kwanza ni Mil 1,000,000 wa pili Sh 750,000 na wa tatu ni 500,000.

“Unaweza kulipia mtandaoni na pia kwa kujiandikisha kupata fomu za ushiriki kwenye maduka ya Dauda sports, Just Fit sports gear Kijitonyama na Mlimani City na kwa Zanzibar zinapatikana kupitia Cataluna Barbershop iliopo Kiembesamaki, Park Hyatt Zanzibar, Cape Town fish market Zanzibar,” alisema Hassan Mussa Ibrahim msemaji wa mbio hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles