29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

NMB kinara mikopo kwa walimu, watumishi

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Benki ya NMB imetajwa kuwa ndio benki pekee nchini iliyotoa mikopo kwa watumishi wa serikali kuu na serikali za mitaa huku walimu wakiwa wanufaidika wakubwa zaidi.

Mwalimu wa shule ya sekondari ya Mwembesongo, Abdula Omary akizungumza jambo wakati wa kongomano la benki ya NMB na walimu lililofanyika mkoani Morogoro.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Marthin Shigela wakati wa kongamano la siku ya walimu lililoandaliwa benki ya NMB na kuwahusisha walimu wote wa mkoa huo pamoja na maafisa elimu.

Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa serikali inatambua mchango wa NMB katika kuwathamini walimu na watumishi wa serikali kuu na serikali za mitaa kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu.

Alisema kuwa mikopo kwa watumishi imekuwa msaada katika kukidhi mahitaji mbalimbali katika ngazi ya familia hata kufanikisha maandalizi yao kwa maisha ya baadaye pale wanapostaafu.

“Natoa rai kwenu walimu kutumia fursa hii kwa kujifunza maswala ya kibenki ikiwemo mikopo, bima, amanana huduma mbalimbali za NMB ambazo zitawasaidia sio tu kupanua uwezo wenu kiuchumi bali pia kujenga utamaduni wa kuweka akiba ili kukithi mahitaji ya dharura pindi yanapojitokeza.”alisema Shigele.

Naye Meneja mwandamizi mikopo kwa watumishi na taasisi za serikali NMB, Emmnuel Mahodanga alisema kuwa benki hiyo imeona ni muhimu kukutana na wadau wake wakubwa katika huduma za kibenki kuzungumza nao na kuwapa maendeleo ya benki yao.

Mahodanga alisema kuwa kongomano hilo linalenga pia kuwapa uwelewa zaidi wa huduma za benki hiyo ambapo wanaamini kupitia walimu zaidi ya 150 watasaidia kupeleka elimu kwa wenzao.

Mmoja wa walimu Grace Njau alisema kongomano hilo limekuwa na tija kwao kwani wametambua fursa na matumizi zaidi ya kidigital kutumia simu kwa kuunganishwa na huduma za NMB.

“Kongomano hili ni fursa kwenu kufahamu mambo mengi ndani ya benki hii na tumeweza kujua huduma nyingine mpya za kidigital ikiwemo kadi maalumu inayoweza mtu kufanya manunuzi sehemu mbalimbali kama super market,”alisema Grace.

Wakati huo huo benki hiyo imekutana na walimu, wakuu wa shule, wakuu wa vyuo na wadau mbalimbali wa elimu Mkoa wa Singida katika kongamano hilo la Siku ya walimu, ambapo Mkuu wa mkoa huo, Dk. Binilith Mahenge ambapo amewataka walimu hiyo kutumia fursa zilizopo kwenye benki hiyo.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa kupitia NMB walimu hao hawana budi kuwekeza kwenye cha alizeti, kutokana na serikali kuweka mpango mkakati mkubwa wa kuboresha kilimo cha zao hilo ambalo limeonekana kuwa na faida kubwa.

“Serikali inatoa ruzuku kwenye kilimo cha alizeti na lengo kuu, likiwa ni nchi kujitosheleza kwa mafuta ya kula.Benki ya NMB nayo inaunga mkono serikali kwa kutoa mikopo kwa wakulima wakiwemo wa zao la alizeti. Kwa hiyo waalimu nawaomba mtafute maeneo ya ardhi, ili muweze kulima zao la alizeti,” alisema Mahenge.

Naye Meneja mwandamizi wa kitengo cha wateja maalumu, Ally Ngingite alisema kuwa NMB imeendelea kuwekeza zaidi katika huduma za kidigital ili kupunguza foleni katika matawi ya benki hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles