24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

NLD chaonya wanachama wake

NA KOKU DAVID, DAR ES SALAAM

CHAMA cha National League For Democracy (NLD) kimewataka wanachama wake wote walioko Zanzibar kutokubali kushiriki katika uchaguzi usio rasmi unaoitwa uchaguzi mkuu wa marudio huko Zanzibar ambao unaonyesha wazi kutokuwa na haki ndani yake.

Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu wa NLD, Tozzy Matwanga,  ambapo aliweka wazi msimamo wao wa kuungana na CUF kuhusu uamuzi wa kutoshirki uchaguzi wa marudio Visiwani humo.

Alisema kitendo kilichofanywa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha cha kufuta uchaguzi ni kuashiria uporaji wa demokrasia na haki ya wapiga kura wa Zanzibar.

Alisema hakuna kifungu cha sheria au katiba kinachomruhusu mwenyekiti wa Tume kufuta uchaguzi.

“Wasimamizi wa uchaguzi wa ndani na nje wenyewe wamekiri kuwa uchaguzi ulikuwa ni huru na wa haki hivyo alichotakiwa Jecha kama Mwenyekiti wa ZEC ni kumaliza kuhesabu kura maeneo yaliyobaki kisha kutangaza mshindi wa urais,” alisema Matwanga.

Alisema NLD ni moja ya wananchama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), hivyo ina jukumu la kuhakikisha haki ya Wazanzibari inalindwa kama walivyoamua kupitia sanduku la kura Oktoba 25, mwaka jana.

“Utawala huu wa kiimara ni hatari kwao kwani wananchi wamechoka, NLD tunahitaji katiba mpya hivyo tunawataka wabunge wetu wa UKAWA na wabunge wote wanaoitakia mema nchi yetu kudai katiba na Tume huru ya Uchaguzi,” alisema Matwanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles