23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Nkurunzinza ataka wakutanishwe na Kagame

BUJUMBULA, Burundi

RAIS wa Burundi, Pierre Nkurunziza amesema kuna mzozo wa wazi kati ya taifa lake na la jirani  la  Rwanda katika kinachoonekana kuwa kudorora zaidi kwa uhusiano baina ya mataifa hayo mawili.

Rwanda na Burundi zimekuwa na uhasama kwa muda sasa, ambapo Rais Nkurunziza anaituhumu Rwanda kuhusika katika jaribio la kutaka kupindua serikali yake mwaka 2015 ambalo lilishindwa.

Katika madai yake Burundi inasema Rwanda iliwafadhili waliohusika na kwamba inatoa hifadhi kwao jambo ambalo taifa hilo  limekuwa likikanusha tuhuma hizo mara kwa mara.

Kufuatia hali hiyo Rais Nkurunziza ameshamwandikia barua Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,  Yoweri Museveni   akisema Rwanda sasa si mshirika tena ndani ya jumuiya bali ni kama adui.

“Rwanda ndiyo nchi pekee katika kanda hii ambayo ndiyo moja wa wahusika wakuu katika kuvuruga uthabiti wa taifa langu na kwa hivyo siichukulii kama taifa mshirika, lakini kama adui ya nchi yangu,” barua hiyo, ambayo inaonesha ilitiwa saini na Rais  Nkurunziza Desemba 4 Desemba mwaka huu inaeleza.

Kiongozi huyo anataka kufanyike mkutano maalum wa EAC wa kujadili mzozo huo kati ya Rwanda na Burundi.

Viongozi wa mataifa ya jumuiya hiyo ambayo kwa sasa inajumuisha Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya, Tanzania na Sudan Kusini wamepangiwa kukutana tena Desemba 27  mwaka huu.

Hii ni baada ya mkutano wao wa hivi karibuni kushindwa kuendelea jijini Arusha kutokana na kutokuwepo kwa ujumbe kutoka Burundi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles