27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

NKAMIA: NAMSUBIRI SPIKA MIAKA SABA YA URAIS


Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM

MBUNGE wa Chemba, Juma Nkamia (CCM), amesema anamsubiri Spika wa Bunge, Job Ndugai, ili aweze kumwambia aache hoja yake binafsi ya kutaka muda wa Rais kuwepo madarakani uongezwe kutoka miaka mitano ya sasa hadi saba.

Akizungumza na MTANZANIA kwa simu juzi, Nkamia alisema anaheshimu kauli ya Rais, Dk. John Magufuli, ambaye pia ni mwenyekiti wake, lakini anangoja uamuzi wa Spika kwa kua alishaandika barua yenye nia ya kuwasilisha hoja hiyo.

Nkamia alisema licha ya mwenyekiti wake (Rais Magufuli) kuingilia kati, lakini Spika ndiye atakayemwambia aache hoja hiyo au laa kama taratibu za Bunge zinavyotaka.

“Nimemsikia Rais akizungumzia hilo lakini nafuata kanuni za Bunge, hivyo Spika atanipa maelekezo ya nini cha kufanya, ndio maana kuna mihimili mitatu ikiwa ni pamoja na Mahakama, Bunge na Serikali kila mmoja una fanya kazi yake,’’ alisema Nkamia.

Januari 13,  mwaka huu Rais Magufuli alifunga mjadala wa hoja hiyo kupitia mazungumzo yake na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (Itikadi na Uenezi), Humphrey Polepole kwamba hana mpango huo.

Polepole alisema, Rais Magufuli alimwelekeza kuwajulisha wanachama wa CCM na Watanzania wote kuwa anasikitishwa na hafurahishwi na mjadala unaoendelea juu kuongezwa kwa kipindi cha urais kutoka miaka 5 iliyowekwa kwa mujibu wa Katiba hadi 7.

“Rais Dk. Magufuli amewataka wanachama wa CCM na umma wa Watanzania kwa ujumla kuupuuza mjadala huo kwa kuwa haujawahi kujadiliwa katika kikao chochote cha chama na pia ni kinyume na katiba ya CCM na Katiba ya nchi,” alisema Polepole.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles