24.6 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

NKAMIA AMVAA DC MBELE YA MKUU WA MKOA

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA


MBUNGE wa Chemba, Juma Nkamia (CCM), amemshambulia Mkuu wa Wilaya hiyo, Simon  Odunga, mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,  Jordan Rugimbana kwa madai kuwa anafanya kazi kwa ubabe.

Wiki iiyopita,   Odunga alinusurika kupigwa na wananchi wa Kijiji cha Mlongia Kata ya Jangalo Tarafa ya Mondo   kwa madai kuwa alitoa lugha ya kuudhi na vitisho kwa wananchi wa kijiji hicho.

Nkamia alliyasema hayo jana mjini hapa wakati akichangia katika kikao cha Kamati ya Ushauri cha Mkoa wa Dodoma (RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Maendeleo Vijijini (Mipango).

Mgeni rasmi katika mktano huo alikuwa ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

 Baada ya Waziri Mkuu kuufungua na kuondoka, ndipo Nkamia alipoanza mapambano ya maneno dhidi ya mkuu huyo wa wilaya.

Nkamia ambaye alipewa nafasi ya kuzungumza alimuomba Mkuu wa Mkoa Rugimbana kutatua migogoro ambayo inasababishwa na baadhi ya viongozi akiwamo Odunga.

Mbunge huyo alimtaka mkuu wa mkoa kuangalia uwezekano wa kutatua migogoro ya ardhi ambayo inaonekana kushamiri kwa kasi katika Mkoa wa Dodoma.

“Sijui wananunuliwa na wawekezaji tena wawekezaji matapeli, nashangaa kuona kijiji kinakuwa na mamlaka ya kugawa zaidi ya ekari 500 wakati kanuni zinaonyesha kijiji kinatakiwa kugawa ekari zisizodi 50.

“Ni mamlaka gani zinazompa Mkuu wa Wilaya kuhamisha mipaka… amekuwa akilazimisha kuhamisha mipaka kutoka sehemu moja kwenda nyingine bila kuwashirikisha wananchi lakini mtu akitaka kuhoji jambo lolote anawekwa ndani,’’ alisema Nkamia

Mbunge huyo wa Chemba, alisema mkuu huyo wa wilaya amekuwa akiendesha shughuli zake kwa ubabe huku akijiita Rais wa Wilaya bila kujua kuwa Rais ni mmoja.

Baada ya mbunge kuzungumza, Mkuu wa Mkoa, Rugimbana alikataa kumpa nafasi kuzungumza DC Odunga na kusema kuwa anaijua migogoro ya ardhi jinsi ilivyo.

“Kimsingi naijua migogoro ya ardhi jinsi ilivyo hivyo tutaangalia jinsi ya kuitatua, hivyo nimewaelewa naomba tuendelee na mambo mengine.

“Nitaomba wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri zote tukutane kwa muda mfupi tuweze kuongea mambo machache,’’ alisema Rugimbana

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,745FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles