22.7 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Njooni mtembelee hifadhi ya RAU-TFS

Na Safina Sarwatt,Moshi

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Wilaya ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro, imesema Hifadhi ya Msitu Asilia wa Rau uliopo Kata ya Njoro Mjini Moshi, imesheheni Vivutio mbalimbali vya Utalii ikiwemo mimea na miti ambayo ni adimu inayopatikana katika eneo hilo pekee.

Hayo yamesemwa Aprili 29,2021 na Mhifadhi Mkuu wa Msitu huo, Godson Ollomi, wakati wa ziara ya siku moja na Waandishi wa Habari pamoja na watumishi wa TFS, waliotembelea hifadhi kwa lengo la kuvitangaza Vivutio vilivyomo katika Msitu huo.

Ollomi amesema hifadhi ya Msitu Asilia wa Rau una fursa nyingi za Utalii zilizopo katika msitu huo lakini haijatangazwa vya kutosha hivyo amewahamasisha wakazi wa Manispaa ya Moshi mkoani humo kuweza kutembelea hifadhi hiyo ili kuweza kujionea vivutio ambavyo havipatikani kwingineko nchini.

“Hifadhi ya Msitu Asilia wa Rau ni miongoni mwa misitu asilia 13 iliyopo hapa nchini Tanzania inayosimamiwa na TFS ambao unachukua hekta 570 za Manispaa ya Moshi,” amesema Ollomi.

Amesema Msitu wa Rau ni msitu wa kipekee ambao una wanyama wengi, mimea na miti ambayo huwezi kuipata katika mahala pengine isipokuwa msitu wa rau.

“Unapofika katikati ya Msitu wa Rau utakutana panya wenye masikio makubwa kama ya tembo ambao hawapatikani katika hifadhi yoyote hapa nchini pia kuna vinyonga weupe, pamoja na ‘mti wa mvule ambao unakasiwa kuwa na umri wa miaka 200 na una urefu wa mita 51 na kipenyo cha mita 3,”amesema.

Aidha, Ollomi amesema kwa sasa TFS wanatarajia kuanza kufungua Utalii wa baiskeli ili waweze kujionea vivutio katika hifadhi hiyo badala ya kusimuliwa tu.

“TFS tuna mkakati sasa wa kufungua utalii wa baiskeli lengo likiwa Ni kuweza kutangaza utalii wa ndani na kujionea urithi wa dunia kwa kuwaona wanyamapori kama sehemu ya kukuza utalii wa ndani,”amesema.

Vilevile Ollomi amewataka Waongoza Watalii kuwatembeza watalii wanaofika kwa ajili ya kuupanda mlima Kilimanjaro kuzuru katika hifadhi ya msitu asilia wa Rau.

Askari Msimamizi Msaidizi wa Hifadhi ya Rau, Shadrack Kirimba, amesema licha ya hifadhi ya msitu wa Rua kuwa na vivutio vingi pia unavyo vyanzo tisa vya chemichemi ya maji ambayo vinawasaidia wakulima kunyweshea mpunga wao.

Kwa upande wao waandishi wa habari ,Kija Elias na Jabir Jonson waliozuru msitu huo asilia uliopo kilometa tatu Kusini Mashariki ya Manispaa ya Moshi wameishukuru TFS kwa kuwaandalia ziara hiyo kwani wameweza kujionea Vivutio lukuki vilivyopo kwenye Msitu huo ikiwemo chemi chemi ya maji ya rangi ya maziwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,283FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles