27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Njombe wapunguza vifo vya wajazito, watoto

Elizabeth Kilindi, Njombe

MKOA wa Njombe umepongezwa kwa kupunguza vifo vya kinamama kutoka 250 kwa vizazi hai laki moja mwaka 2005 hadi vifo 94.8 huku vifo vya  watoto walio chini ya miaka mitano vikitoka 51 hadi vifo viwili kwa kila vizazi hai 1,000 Disemba 2019.

Pongezi hizo zilitolewa jana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jjinsia Wazee na Watoto, Faustine Ndugulile, akiwa mkoani hapa kwenye ziara ya siku tatu ya kikazi.

Alisema mama mjamzito anapaswa kuishi na ujauzito salama na usiwe sababu ya kukatisha maisha yake.

“Niwapongeze sana Serikali Mkoa wa Njombe kwa kukabiliana na vifo vya mama na mtoto, tunapaswa kujua ujauzito si ugonjwa hivyo tusiruhusu kukatisha maisha ya mama mjamzito, anatakiwa aishi,”alisema Ndugulile.

Awali akisoma taarifa ya mwenendo wa vifo vitokanavyo na uzazi na watoto chini ya miaka mitano, Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Njombe, Manyanza Mponeja, alisema wamefanikiwa kupunguza vifo hivyo kwa kutumia vituo vya kutolea huduma za afya katika maeneo ya mijini na vijijini.

Alisema mkoa umeweka malengo ya uboreshaji wa huduma za virusi vya Ukimwi na Ukimwi kwa kuongeza vituo vya kutolea huduma kutoka 112 hadi kufikia 130 Disemba 2020.

“Vile vile tunaendekea kuboresha vituo vyote 258 vinavyotoa huduma za kinga ya maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kama sehemu ya huduma katika Kliniki za Uzazi na Mtoto (RCH) ili viweze kutoa tiba na mafunzo kwa watu wenye maambukizi ya VVU”alisema Mponeja.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka, alishauri kuwepo na utafiti wa kina kuhusu takwimu zinazoeleza juu maambukizi ya VVU pamoja na suala la udumavu katika mkoa wa Njombe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles