29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Njia ya Kidia yatengewa Sh mil 200

Na Ramadhani Hassan, Dodoma

SERIKALI imesema katika maandalizi ya kufungua njia ya wageni mashuhuri (VIP) ya Kidia yenye urefu wa kilometa 25, imetenga Sh milioni 200 kwa mwaka 2020/21.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni Dodoma jana na Wizara ya Maliasili na Utalii, wakati ikijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Mmasi (CCM).

Esther katika swali lake alidai kwamba  wananchi wa Kata ya Old Moshi Mashariki kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakingoja uzinduzi wa njia ya VIP kwa wageni waendao kupanda Mlima Kilimanjaro.

Alihoji ni kwanini Serikali isione umuhimu wa kutekeleza azma hiyo iliyodumu kwa muda mrefu sasa.

Ikijibu swali hilo, Wizara ya Maliasili na Utalii ilieleza kuwa kupitia Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa), ilishaona umuhimu wa kufungua njia ya Kidia itakayotumika kwa wageni maarufu (VIP) watakaokuwa wanapanda Mlima Kilimanjaro.

Kutokana na umuhimu wa njia hiyo, shirika limeiweka kwenye mpango wa jumla wa usimamizi wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro (General Management Plan – GMP) wa mwaka 2016-2026.

Ilieleza katika maandalizi ya kufungua njia hiyo, pia Sh milioni 230 zimetengwa kwa ujenzi wa ofisi ya kupokea na kuhudumia wageni, lango pamoja na kutengeneza njia (trail) ya kupandia mlima kuanzia Kidia.

“Kuzinduliwa kwa njia hiyo kutaongeza mapato ya Serikali kupitia utalii, lakini pia kutaongeza fursa kwa wananchi wa Kata ya Old Moshi Mashariki kufanya biashara kwa watalii, mawakala wa utalii na watoa huduma ya utalii watakaokuwa wanatumia njia hiyo,” ilisema wizara hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles