24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

NJIA KUMI MADHUBUTI ZITAZOOKOA FEDHA, KUKUPA AFYA

fitness guys biking in gym

NA DK. FREDIRICK L.MASHILI,

KUNA njia nyingi mno za kupunguza matumizi ya fedha kwa zaidi ya asilimia 50, huku ukiendelea kuneemeka kwa kuwa na afya njema.

Leo nitakupa mambo ya kuzingatia ili kufanikisha jambo hilo.

  1. Kunywa kistaarabu

Waingereza wanasema; ‘drink responsibly.’ Kama wewe ni mpenzi wa vinywaji vyenye kilevi nadhani ni wakati mwafaka kurejea viwango na kiasi cha pombe kinachokubalika kiafya na kushauriwa na wataalamu wa afya. Hii haitakusaidia tu kubana matumizi, bali pia kudumisha afya na kujikinga na magonjwa. Vipimo viwili vya kilevi kwa wanaume na kipimo kimoja kwa wanawake. Kipimo kimoja cha bia ya kawaida ni mfano wa chupa moja ndogo na kipimo kimoja cha mvinyo ni mfano wa glasi moja ya mvinyo.

Kwa maana hiyo hutahitajika kutumia fedha nyingi kununua chupa mbili za bia kama ambavyo ungetumia endapo ungekunywa chupa kumi.

 Epuka kunywa katika makundi

Hii si uchoyo, bali ni njia madhubuti itayokuwezesha kutimiza kilichotajwa hapo juu. Kunywa pombe katika makundi hukuongezea uwezekano wa kunywa pombe nyingi zaidi ya ulivyopanga na kujikuta ukihatarisha afya na mifuko yako. Jenga tabia ya kunywa na marafiki wachache ambao pia wana malengo kama yako. Hii itakufanya kuzingatia viwango vinavyokubalika na kukuepusha na kutumia fedha nyingi bila sababu.

      3. Badilisha sehemu za kujumuika (networking)

Gym ni sehemu mbadala ya kukutana na marafiki

Bado liko kundi kubwa la watu linaloamini kwamba kujumuika na marafiki huweza kutokea baa au sehemu za starehe pekee. Huenda kukawa na ukweli lakini baa si sehemu pekee ya kujumuika.

Katika kipindi cha mwaka huu hebu jaribu kufanya mabadiliko kwa kufikiria sehemu tofauti za kujumuika. Sehemu za mazoezi (gyms, fitness na sports clubs) ni sehemu nzuri pia za kujumuika, wakati huo huo ukipata fursa ya kufanya mazoezi. Jaribu kutengeneza mitandao katika sehemu za ibada, michezo na mazoezi, kama mbadala wa kutengeneza mitandao hii baa au sehemu za vinywaji peke yake. Sehemu hizi mbadala hutoa fursa zenye faida kiafya na kiuchumi.

  1. Beba chakula kutoka nyumbani uendapo kazini

Chakula kilichoandaliwa nyumbani ni kisafi na bora zaidi.

Licha ya kubana matumizi, mlo ulioandaliwa nyumbani huwa na faida nyingi kiafya. Mara nyingi ni chakula kilichoandaliwa katika hali ya usafi, pia kilichoandaliwa kutokana na mahitaji yako. Kama umewahi kushauriwa na daktari kupunguza chumvi katika chakula chako, kula matunda na mboga mboga kwa wingi na hata kupuguza kiasi cha sukari na mafuta mabaya kwenye milo yako–kuandaa chakula chako cha mchana nyumbani ndiyo jibu.

Kubeba chakula kutoka nyumbani pia hukupunguzia adha ya kupoteza muda kwa kusimama katika foleni kusubiri kuhudumiwa. Juu ya yote, chakula kilichoandaliwa nyumbani kina gharama nafuu kuliko kile utakachonunua hotelini au kwenye kantini ya kazini.

  1. Tembea, tumia baiskeli au usafiri wa pamoja unapotoka nyumbani

Kutumia baiskeli hukupa fursa ya kufanya mazoezi, kuhifadhi mazingira na kubana matumizi kwa wakati mmoja.

Kama unaishi karibu na sehemu yako ya kazi, usisite kutembea au kutumia baiskeli kwenda kazini. Tafiti zinaonyesha kwamba watu wanaotembea au kutumia baiskeli huwa na afya bora na huishi maisha marefu kuliko wale wanaotumia magari. Kama unaishi mbali, tumia usafiri wa pamoja kama vile mabasi ya mwendokasi au daladala za kawaida. Kutumia usafiri wa pamoja kunapunguza uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na moshi wa magari. Hii hutufanya tuishi kwenye mazingira safi. Kutumia usafiri wa pamoja pia hupunguza msongamano wa magari na kutufanya tufike kazini mapema. Juu ya yote kutembea, kutumia baiskeli au usafiri wa jumuiya/pamoja, hupunguza matumizi kwa kiasi kikubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles