27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Njia hii itakupa sababu ya kufurahia uhusiano wako

KILA mtu kwa nafasi yake anahitaji kufurahi katika mahusiano yake. Hakuna asiyependa hali hiyo. Mapenzi ni raha, furaha na ni suala la amani ya nafsi, sasa kwanini mtu achukie?

    Ila mbali na ukweli huo ni watu wachache sana wanaofurahia mahusiano yao ya kimapenzi ukiachana na zile siku za mwanzo za upya wa penzi lao.

    Zile siku ambazo kiujumla ni lazima tu wahusika wafurahie kutokana na upya na ugeni wa kila mmoja kwa mwenzake.

  Watu wengi baada ya kupitisha miezi kadhaa katika mahusiano yao huanza kujikuta katika hali ya tofauti kiasi. Hali ya kutofurahia kwa ukamili mahusiano yao kama ilivyokuwa mwanzo. Katika hili kuna sababu nyingi. Ila leo tutaenda kuiona moja tu.

   Wapenzi wengi hujikuta wakipoteza raha na amani katika mahusiano yao kutokana na kupenda kuchukulia kila tendo au neno la mwenzake katika uzito wa juu. Hapo bila kuangalia, muhusika aliongea au alitenda jambo hilo katika hali gani. Kama ni ya utani, alidhamiria au bila kujua. Wao hilo hapana.

   Kutokana na kuchukulia mambo katika mtindo huo bila kuangalia wahusika wametenda kwa namna gani au kwa sababu gani, wengi ya wapenzi wamejikuta wakipoteza morali na ile hali ya furaha waliyokuwa nayo kwa wapenzi wao.

   Ni vyema ikaeleweka kuwa kila binadamu ana tabia ambayo inampa utofauti na mtu mwingine. Unaweza kuwa umefanana na fulani karibu kwa kila kitu ila kuna kitu ambacho ni lazima tu utakuwa umetofautiana naye. Hiyo haijalishi ni katika mazungumzo au matendo. Sasa hapa ndiyo kuna leta shida kidogo.

  Wengi baada ya kuwa na kina fulani katika mahusiano yao wanapenda wafanane nao karibu kwa kila kitu ili aweze kujiridhisha katika nafsi yake kuwa aliye naye ndiyo chaguo lake kamili. Kitu ambacho hakiwezekani.

  Unakuta anaanza kumfuatilia kwa kina na kutoa tafsiri kuanzia katika maongezi yake mpaka matendo yake. Ukiwa hivi kwa mwenzako ni lazima tu utampata na kasoro.

 Na hizi kasoro kimsingi ukiendelea kuzitafakari katika mrengo wa kuhukumu ni lazima tu katika mapenzi yenu kuanze kujitokeza dosari.

   Ndiyo, ni vyema tukawajua wapenzi wetu ili kuwa na amani na kuwa na uwezo wa kuwapa raha na faraja pia. Lakini siyo katika mtindo huu.

  Kitu au binadamu yoyote ukianza kuwa na mashaka naye ni lazima tu utaona matendo yatakayokufanya uhisi unaibiwa, unadharaulika au ana mtazamo tofauti katika mapenzi yenu tofauti na ulio nao.

 Na zao kuu la fikra za namna hii ni kumfuatilia sana mpenzi wako kana kwamba umeombwa utoe orodha ya matendo na maneno yake mahala. Katika aina hii ya maisha huwezi kufurahia mapenzi.

Kila mtu kwako atakuwa hafai. Maana katika ufuatiliaji wako wa namna hiyo katu huwezi kumkuta bila kitu cha kukufanya upatwe mashaka. Na hiyo si kwa mpenzi au mke wako tu.

  Ni kwa kila mtu ukifanya hivyo basi utakuta kuna vitu vya kukupa mashaka katika maisha yako. Ebu kuanzia leo anza kuwa na wasi wasi na rafiki zako wanaokuja nyumbani kwako.

 Tengeneza picha mmoja wao anakuchukulia dada yako au mkeo kisha anza kuchunguza kwa kina kabisa. Ni lazima tu utapata viunganishi vya kumtia hatiani hata kama siyo.

    Wasiwasi ukiuendekeza huleta picha kamili hata kama si halisi. Jiamini kwa mpenzi wako. Si ulimtongoza na akakukubali bila kumshurutisha? Sasa hofu ya nini.  

   Au huamni matendo yako kwake kama yanamfurahisha? Sasa dawa si kuwa na wasi wasi badala yake ni kumfanyia mwenzako vitendo vya kumpa raha na furaha.

Wasi wasi wako siyo dawa wala kinga ni mabadiliko yako tu ndiyo yatakayomfurahisha. Ukimbana ama kumchunguza mwenzako kupita kiasi siyo tu utajikuta ukiingia naye katika migogoro ya mara kwa mara ila pia hata mahusiano yenu yataanza kukosa ladha na msisimko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles