24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Njia bora za kuishi na mpenzi aliye mbali

MAPENZI ni hisia ambazo hazizuiliwi na mipaka ya nchi ama mabara katika kusafiri kwake. Hisia ambazo zinapenya mbele ya uzio wa dini, kabila rangi na vipato.

Kawaida ya hisia za mapenzi ni kutengeneza daraja na siyo kujenga ukuta kwa watu. Kama mtu ana hisia halisi za mapenzi juu ya fulani, hujikuta akimthamini, kumjali na kumtakia mengi ya heri bila kujali rangi wala kipato chake na sifa zinginezo.

Watu wengi kwa kutofahamu huamini wapenzi wao wakisafiri na kukaa mbali kwa muda fulani basi inaweza kuwa chanzo cha wao kutopendwa na kuhitajika tena.

Katika dunia ya sasa, yenye kila aina ya nyenzo cha za mawasiliano, kuwaza hivyo ni kosa kubwa. Japo ni muhimu wapenzi kuonana ana kwa ana (Physically) ila inapotokea kutoonana, tena kwa sababu za msingi maana yake siyo imefika tamati ya uhusiano wenu.

 Mapenzi ni hisia. Ili mwenzako akujali na akuthamini, inabidi ucheze na akili yake hali itakayoshawishi hisia zake zikutazame wewe katika namna fulani bora.

Mwenzako akikuona wa thamani, bora na mwenye vingi vya kujivunia, ndiyo anaweza kuona wengi pengine na kuwasifia kila binadamu ana tamaa, tunatofautiana katika namna ya zikiachia na kuzidhibiti ila wewe daima kwake utabaki kuwa bora na wa thamani.

Kuna wengi wanaonana kila siku, wengine wanalala chumba kimoja ndani ya shuka moja ila hawana mshikamano wa kweli kama wale ambao wanaoishi mbali mbali.

Kwa sababu wameshindwa kushikana kihisia vile inavyotakikana. Jiulize kwa makini. Mwenzake anakutazama vipi? Anakuona ni binadamu tu au anakoshwa hasa na unavyomtendea, unavyomjali, unavyomfurahisha na kumpa raha na furaha?

 Kama kupitia matendo na kauli yako unamfanya mwenzako akuone wa pekee, mtu ambaye una vingi vya kujivunia, basi anaweza kuona watu wengi ila kwako akajiona amebahatika sana kuwa na wewe.

 Inachotakiwa tu kwa kuwa mwenzako yuko mbali ni kudumisha mawasiliano. Yaani muongee ama mchati ila pia katika huko kuchati ama kuongea, uhakikishe maongezi yenu mara nyingi yawe ya kuwapa furaha, amani na msisimko.

Inabidi kwa gharama yoyote ujiepushe na migogoro isiyo na tija  kupitia kuwasiliana kwenu. Kwa watu walio mbali mbali migogoro ya kila siku inachefua kwa kasi hisia zao na kwa kuwa yuko mbali na mwenzake, anaweza kujikuta anakabiliwa na wingi wa fikra hasi hali inayoweza kumfanya atafute sehemu ya kutua matatizo yake walau kwa muda.

 Ukiwa unachati mara nyingi pendelea kuchati naye juu ya matamanio yake na vitu anavyopenda. Zungumza naye mambo unayojua huwa yanampa raha na hamasa sana ama katika maisha au katika mahusiano.

 Utabaki na udhibiti wa mwenzako hata akiwa mbali kama utafanikiwa kuamsha na kusisimua hisia zake za namna nzuri hata akiwa mbali.

 Tatizo la wengi ni kwamba wakiwa mbali na wapenzi wao hujikuta wakiacha kujiamini kabisa hali inayopelekea kila siku kuwatuhumu wenzao katika masuala mbali mbali ya usaliti hatua inayoleta migogoro ya mara kwa mara katika uhusiano husika.

Hali hii inapoendelea husababisha hata msisimko wa wenzao kwao kupungua kitu kinachovunja muunganiko wa kihisia (Breaking emotional connection) na hivyo wenzao kuamua kuanzisha mahusiano mengine kwa sababu haya waliokuwapo hayawapi tena sababu ya furaha wala matarajio mema.

Kuna aina ya vi mgogoro vinavyochochea hali ya mapenzi kwa mwenzako ila migogoro ya kila siku hukera na kufanya mtu ajutie kuwasiliana na wewe kitu kinachofanya pia achukie kuwa na wewe katika maisha yake.

Vimgogoro vinavyotokana na kudeka, mfano, umempigia mwenzako simu mida ambayo una amini huwa yuko huru na akachelewa sana kupokea, hapa ukijifanya kukasirika na kususa kidogo, sio mbaya sana.

Itamfanya mwenzako akubembeleze na kwa namna fulani atahisi (feel) kosa lake. Kitu hiki kitazidi kumfanya awe makini na wewe hali itakayoimarisha mahusiano yenu.

 Ila siyo unajua mwenzako mida hiyo anaweza kuwa busy na majukumu ya kikazi kisha akaacha kupokea ama akachelewa kupokea simu, ukaanza kulaumu, kutuhumu hata na kutoa kauli chafu.

Siyo kitu kizuri, maana kinakera na kuumiza. Unapompigia simu mida ya kazi inabidi ufahamu huwezi kupata mazingatio ya kutosha (enough attention) kama ambavyo ukimpigia mida ambayo yuko huru.

Hivyo kipindi ambacho yuko kazini ni ngumu sana mwenzako kuwa na mwitikio kamili wa kimapenzi. Elewa hilo na ninakutakia msimu mwema wa wapendanao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles