28.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Niyonzima kufungwa miaka mingine miwili Simba

Na ZAINAB IDDY- DAR ES SALAAM

KIUNGO wa kimataifa wa Rwanda anayeichezea Simba, Haruna Niyonzima, ameweka wazi kuwa anatarajia kusaini kandarasi mpya ya miaka miwili na kikosi hicho, mara baada ya mkataba wake wa sasa kufika tamati mwishoni mwa msimu huu.

Niyonzima alijiunga na Simba akitokea Yanga msimu wa 2017/18.

Mnyarwanda huyo alitua Simba kwa kitita cha dola 60,000 (Sh milioni 120 za Tanzania), pamoja na kulipwa mshahara wa Sh milioni 6 kwa mwezi.

Akizungumza na MTANZANIA, Niyonzima, alisema mkataba wake unaelekea kufikia ukingoni, lakini tayari mabosi zake wameonyesha nia ya kuendelea naye.

“Kocha ameshaniambia anahitaji kuona nabaki katika kikosi chake, jambo lililoungwa mkono na mabosi pia, hivyo mara baada ya mkataba wangu wa sasa kumalizika nitasaini mwingine.

“Mipango yangu ni kuongeza wa miaka miwili tu kwani nimeshakaa sana Tanzania na sihitaji soka langu limalizikie hapa, baada ya mkataba mpya nitakaoingia nao kumalizika nitarejea nyumbani,” alisema Niyonzima ambaye kwa sasa ameonekana kurejea katika kiwango cha juu, baada ya kutokuwa fiti kutokana na majeraha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,908FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles