25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

NIYONZIMA AWATULIZA MASHABIKI YANGA

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM


niyonzima-3NAHODHA wa timu ya Yanga, Haruna Niyonzima, amewaomba mashabiki wa timu hiyo kusahau kilichotokea katika michuano ya Kombe la Mapinduzi na badala yake waelekeze nguvu katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga iliondoshwa katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 4-2 na watani wao wa jadi Simba.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Rwanda, aliliambia MTANZANIA jana kuwa baada ya kutolewa kwenye Kombe la Mapinduzi huu ni wakati mwafaka wa kuungana kwa pamoja ili kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri ligi kuu.

“Kwa sasa hatuna muda wa kupoteza kwa kukumbuka mambo yaliyopita kwani hatuwezi kubadilisha kilichotokea, jambo la msingi ni mashabiki kuelekeza nguvu zao ligi kuu,” alisema Niyonzima.

Aidha, Niyonzima aliwaomba mashabiki kumpa muda kocha wao Mzambia, George Lwandamina kwani bado ni mapema sana kuanza kujadili uwezo wake hasa baada ya kupoteza mechi kubwa dhidi ya Simba na Azam.

“Lwandamina ni kocha mzuri akiendelea kukinoa kikosi chetu, hivyo ni jukumu letu kumuunga mkono na kuheshimu anachokifanya,” alisema Niyonzima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles