22.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

Niyonzima arejea kuongeza makali Yanga

harunaaNA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

KIUNGO mchezeshaji wa Yanga, Haruna Niyonzima, amerejea kuiongezea makali timu hiyo baada ya kuikosa mechi ngumu dhidi ya Azam FC iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Jumamosi iliyopita Yanga ilijikuta ikipunguzwa na kasi na Azam katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kiungo huyo raia wa Rwanda ambaye ni tishio Ligi Kuu na injini ya kikosi cha Yanga kutokana na umahiri wake wa kuichezesha timu na kuiwezesha kufikia mafanikio ya kukaa kileleni kwa muda mrefu.

Meneja wa timu hiyo, Hafidh Salehe, aliliambia MTANZANIA jana kuwa kiungo huyo tayari amerejea nchini baada ya kumalizika kwa shughuli yake ya ndoa iliyofanyika wiki iliyopita nchini kwao Rwanda.

Alisema kikosi cha Yanga kitavaana na Toto Africans kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kikiwa na kasi yake ya ushindi iliyozoeleka.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles