22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 1, 2022

NITAPAMBANA NA MAKONDA  UBUNGE NYAMAGANA – MABULA

 

MWANZA     

Na CLARA MATIMO

MBUNGE wa   Nyamagana, Stanslaus Mabula, (CCM) amesema hana hofu kuhusu taarifa za uamuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda    kuwa atawania ubunge katika jimbo hilo.

Alisema   atachuana na wagombea wengine wote watakaojitokeza.

Alikuwa akizungumza juzi katika mahojiano maalum wakati alipotembelea ofisi ya Kanda ya Ziwa ya New Habari (2006) Ltd wachapaji wa magazeti ya MTANZANIA, Dimba, Bingwa na Rai.

Mabula alisema ameamua kutangaza nia yake ya kugombea tena kutokana na watu wengi kumzushia kuwa hatogombea.

Baadhi ya wanaotajwa kuwania ubunge katika jimbo hilo pamoja na   Makonda ni  Robert Masunya, Joseph Kahungwa, Raphael Shilatu Dk. Barnabas Mbogo   na aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema, Ezekiel Wenje.

“Naomba nieleze wazi kuwa bado nina nia ya kuwania ubunge tena…  nimesikia wengi wakipita na wengine wakisemea mabarazani kuwa watawania.

“Nimemsikia ndugu yangu Makonda pia akitajwa kuja … ni haki yao wakija nitapambana nao kwa kuzingatia kanuni na taratibu za chama, hakuna ninaemuogopa,” alisema.

Mabula alisema hamuogopi mgombea yoyote   ndani ya CCM na nje ya chama ambaye atajitokeza kuomba kuchaguliwa na wanachi .

Hata hivyo aliwaomba wananchi  kutulia wangoje muda muafaka wa uchaguzi ili wapambane kwenye kinyang’anyiro.

“Wakati nagombea ubunge mwaka 2015 nilipambana na mtu aliyekuwa anakubalika sana kwa wapiga kura na mpinzani mwenye nguvu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ezekiel Wenje.

“Huyo anatosha kutoa picha kwamba kuwa maarufu sana hakukufanyi kushinda uchaguzi kwenye jimbo hili,” alisema.

Alisema uamuzi wa mwisho upo kwa wananchi wanaopiga kura, naye akiwa mbunge   anaamini kuwa atapimwa kutokana na utendaji wa kazi zake na namna alivyokamilisha ilani ya uchaguzi jimboni.

Alisema kwa sasa  anaendelea na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya maji safi na salama, elimu, afya na ujenzi wa miundombinu ya barabara.

“Unajua jimbo la Nyamagana tumechelewa kupata maendeleo ikiwamo kutokuwa na kituo cha afya  kwa miaka mingi, sababu wabunge wote walionitangulia walikaa madarakani kwa awamu moja tu.

“Hili niwaombe wananchi kuliangalia maana unakuta mbunge hajamaliza hata mipango waliyojiwekea anaachwa na kuchaguliwa mwingine na mambo yanakwamia njiani,”alifafanua Mabula.

Alisema hali hiyo ya kuwaweka madarakani kwa awamu moja wabunge wa   Nyamagana  ikiendelea itasababisha wabunge wanaoingia madarakani kufanya kazi ya kujikusanyia fedha jambo ambalo si la busara.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Nukuu ya Hayati Mwl.Nyerere:Ubaguzi una sheria yake ni sawasawa na Kula nyama ya mtu,ukila nyama ya mtu hawezi kuacha mkiwabagua wachaga kwa kusema sisi si wa moja na wachaga hamna ishirini hapo mnaendelea,na baadae mtajikuta kuwa hata nyingi kumbe siwamoja – sasa mtapigana Fimbo wenyewe Nyamagana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,373FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles