23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

NIT YASHAURIWA KUZALISHA WATAALAMU WA ANGA

nit

Na ESTHER MNYIKA- DAR ES SALAAM

CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), kimetakiwa kuchangamkia fursa za kuandaa wataalamu wa kada mbalimbali za usafirishaji wa anga ili kuinua sekta hiyo na kuiwezesha nchi kujulikana kimataifa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Baraza la Chuo hicho, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, alisema kuzalisha wataalamu pekee haitoshi, bali ni jukumu la uongozi wa Baraza hilo kuhakikisha wanawasaidia wataalamu hao kwa kuwaunganisha na mashirika makubwa ya usafirishaji, lengo ni kuwajengea uwezo na kuwatambulisha kimataifa.

“Tayarisheni wataalamu na muwakutanishe na wakurugenzi wakuu wa Makampuni kama Emirates, Qatar na Etihad, ili kuwawezesha kupata fursa kirahisi na wao kuweza kuonekana kimataifa,” alisema Profesa Mbarawa.

Aliongeza kuwa, Chuo kinahitaji kuchukua wafanyakazi kutoka Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), ili kutoa mafunzo kwao kwa ajili ya kuzalisha wataalamu wenye ujuzi na uwezo wa kujenga miradi mbalimbali, ikiwamo ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge).

“Msipotumia fursa kama hizi za kuandaa wataalamu wa mbalimbali, tutakosa wataalamu wazawa wa miradi mikubwa na kuanza kulalamika kuwa chuo kipo lakini hakithaminiki, kumbe mwanzoni tulishindwa kujipanga,” alifafanua Profesa Mbarawa.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles