24.3 C
Dar es Salaam
Monday, September 16, 2024

Contact us: [email protected]

NIT chajivunia kozi za kimkakati

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimesema miradi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa na Serikali nchini imetoa hamasa kwa Watanzania wengi kuchangamkia fursa za kozi mbalimbali chuoni hapo.

Maofisa udahili wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mwachenga Singa (Kulia) na Rodrick Mero wakiwahudumia wakazi wa Dar es Salaam waliotembelea banda la chuo hucho kwenye Maonesho ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia.

Akizungumza Dar es Salaam Julai 18,2023 wakati wa maonesho ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayoratibiwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Kaimu Ofisa Uhusiano wa chuo hicho, Juma Mandai, amesema huwa wanafanya tafiti mbalimbali kujua mahitaji yaliyopo katika soko la ajira.

Amesema kozi hizo ni za huduma wa usafiri wa reli, meli, anga, usimamizi wa bandari na usafiri wa anga ambapo kuna kozi za uhandisi wa ndege, wahudumu wa ndege na nyingine.

“Maboresho yanayofanywa katika sekta ya uchukuzi yanahitaji watalaam mbalimbali hivyo, yametusukuma kuwa na kozi za kimkakati zinazozingatia mahitaji ya soko la ajira ambazo zimewavutia Watanzania wengi kuja kusoma katika chuo chetu.

“Hatuanzishi kozi ili mradi tuwe na kozi nyingi, huwa tunaangalia vipaumbele vya Serikali na mahitaji ya soko la ajira, kwahiyo zinawavutia watu wengi hata waliotembelea katika banda letu,” amesema Mandai.

Aidha amesema katika maonesho hayo pia wanafanya udahili wa wanafunzi, wanatoa taarifa za program zinazotolewa na chuo hicho na ushauri elekezi.

Ofisa huyo amesema pia wameanzisha kozi mpya ya Shahada ya Uzamili katika Uhandisi wa Mitambo na kufanya idadi ya kozi za shahada ya uzamili kufikia tatu.

“Chuo kinakua lakini pia tunahitaji wabobezi katika fani ya uhandisi wa mitambo, kwahiyo tunaendelea kuongeza kozi za ‘masters’ ili kupata wataalam wabobezi zaidi,” amesema.

Mmoja wa wahitimu wa kidato cha sita aliyetembelea banda la chuo hicho, Junior Cliford, amesema chuo hicho kina kozi nyingi za kipekee na kwamba amevutiwa kusoma uhandisi wa ndege.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles