22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Nissan wazindua Navara Single Cab

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya Magari ya Nissan Tanzania imetambulisha gari jipya la Navara Single Cab ikisema lina mifumo inayoiwezesha kutumika katika sehemu yoyote.

Mkurugenzi Mkuu wa Nissan Tanzania, Mark Van Rooyen, akizungumza wakati wa kutambulisha gari jipya aina ya Navara Single Cabin. Kulia ni Meneja Masoko na Mauzo, Alfred Minja.

Akizungumza wakati wa kutambulisha gari hilo Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni hiyo, Alfred Minja, amesema limetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu inayoliwezesha kudumu kwa muda mrefu.

“Hili ni toleo la 2021 na ni gari ambayo inaweza kwenda katika sehemu yoyote Tanzania na inaweza kufanya kazi katika sekta zote, linaweza kutumika katika ujenzi wa barabara, kwenye sekta za kilimo, madini ambako kumekuwa na uhitaji katika soko,” amesema Minja.

Amesema pia ukubwa wa tanki la mafuta ni lita 80 ambazo zinaweza kutumika kwa zaidi ya kilomita 1,000 na kwamba bei yake ni Dola za Marekani 27,500 sawa na Sh milioni 63.8.

Aidha amesema gari hilo hufanyiwa service bure kwa miaka miwili na kwamba wanatoa dhamana ya miaka mitatu ambapo wanakadiria litakuwa limetembea kilomita 100,000.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Nissan Tanzania, Mark Van Rooyen, amesema wataendelea kubuni magari mbalimbali yenye ubora wa hali ya juu ili kukidhi mahitaji ya wateja wao.

Kampuni hiyo imetoa fursa za ajira kwa Watanzania na kupitia sera ya kusaidia jamii imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kwa jamii kama vile kwenye sekta ya elimu na afya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles