23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Nishati inaakisi Kauli Mbiu ya Maonesho ya Sabasaba- Mahimbali

Teresia Mhagama na Zuena Msuya, Dar

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali amesema sekta ya nishati inaakisi kauli mbiu ya Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara ambayo ni Uchumi wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu.

Mahimbali alisema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea baadhi ya mabanda ya washiriki wa Maonesho hayo katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, mkoani Dar es Salaam, Julai 4, 2021, ambapo aliambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali (kushoto) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah vitabu vya Sera ya Nishati pamoja Mpango Kabambe wa Umeme mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Nishati katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika jijini Dar es Salaam, Julai 4,2021.

Alifafanua kuwa nishati inaakisi kauli mbiu ya Maonyesho hayo kwa kuwa vitu vyote vilivyolengwa katika kauli mbiu hiyo vinategemea zaidi uwepo wa nishati ya uhakika katika utekelezaji wake.

“Nimefarijika sana kutembelea maonesho haya ya Sabasaba, nimewasikiliza wafanyabiashara kila mmoja kwa nafasi yake amekuwa  akizungumzia nishati ya Umeme kwa namna ambavyo  anaitumia kuboresha Biashara yake kwa namna moja ama nyingine kwa maeneo ya vijijini ni Mijini”, alisema Mahimbali

Aliongeza kuwa, inadhihirisha wazi kuwa nishati ya Umeme ni mkombozi mkubwa wa ukuaji wa uchumi wa nchi na mwananchi mmoja mmoja.

Aidha aliwaasa watanzania kujitokeza kwa wingi kutembelea Banda la Nishati pamoja na Taasisi zake, ili kuona, kujifunza na kupata uelewa zaidi juu ya shughuli zinazofanywa na wizara pamoja na Taasisi zake.

Vilevile aliwaeleza watanzania kuwa wafike katika mabanda hayo ili kuona mfano wa bwawa kubwa la kuzalisha umeme wa megawati 2,115 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji, pamoja na kupata maelezo ya namna mradi huo unavyotekelezwa na hatua iliyofikiwa hadi sasa katika ujenzi wake.

Aliongeza kuwa katika maonesho hayo, watanzania wataona namna ambavyo Joto Ardhi inavyozalisha umeme kwa kutumia mvuke unaotoka chini ya ardhi.

Pia, aliwakumbusha watanzania kutumia nishati ya Umeme katika kujiletea maendeleo kwa kuwa serikali inatumia nguvu kubwa kuhakikisha kuwa nishati hiyo inasambazwa nchi nzima kwa gharama nafuu.

Sambasamba na hilo, watapata maelezo kwa kina kuhusu gharama za kunganishiwa umeme katika nyumba kazoo katika maeneo mbalimbali nchini, na matumizi sahihi ya umeme.

Akiwa katika viwanja hivyo vya Mwalimu Nyerere, Mahimbali alitembelea mabanda mbalimbali ikiwepo la Wizara ya Nishati na taasisi zilizochini yake ambazo ni Shirika la Umeme Tanzania( TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Kampuni ya Uendelezaji Joto Ardhi ( TGDC), Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja( PBPA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Mamlaka ua Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles