27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

NIMR kufanya utafiti wa ukubwa wa tatizo la nguvu za kiume nchini

Aveline  Kitomary – Dar es Salaam

TAASISI ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), wanatarajia kuanza kufanya utafiti wa ukubwa wa tatizo la nguvu za kiume katika sehemu mbalimbali nchini.

Akizungumza na MTANZANIA  katika mahojiano maalum, Mkurugenzi wa Kuratibu na kukuza utafiti, Dk Paul Kazyoba, alisema utafiti huo utaanza mwanzoni mwa mwezi  Machi.

“Tunachotaka kufanya ni kuangalia ukubwa wa tatizo ukoje hasa katika mkoa wa Dar es Salaam, watu wanalalamika lakini inawezekana kuwa sio Dar es Salaam tu, watu wanaweza wakaongea sana lakini ukienda  kwenye takwimu hali inaweza ikawa tofauti na  wanavyongea.

Dk Kazyoba alieleza kuwa katika utafiti huo wataangali zaidi chanzo cha ukosefu wa nguvu za kume ,muda wa tatizo kuanza na tiba ambazo zinaweza kumsaidia mhusika.

“Tukizungumzia nguvu za kiume kuna mambo mengi lazima tuulize imeanza lini au kama alizaliwa akiwa na shida hiyo tutaangalia vitu vyote ambavyo viliweza kuanzaisha tatizo, yapo mambo yanayosababisha  mfano kupanda kwa sukari, msongo wa mawazo ,tatizo la kuzaliwa nayo, aina ya chakula wengine wanatatizo la kisaikolojia tunataraijia kuanza utafiti wa jumla kuanzia mwezi wa tatu,”alibainisha .

Aliwashauri jamii kuepukana na matumizi ya dawa hasa za kuongeza nguvu za kiume ambazo hazijapimwa na kusajiliwa kisheria.

“Madhara ya matumizi ya dawa ambayo haijapimwa au kuangaliwa usalama, maana yake unajitoa muhanga kupata tatizo lingine kubwa kuliko kutibu ulilonalo.

“Kitu cha kwanza dawa zenye sumu nyingi inachoweza kuharibu ni figo, huwezi chukua tu dawa ukanywa, hata dawa zinazotolewa hospitali ukitumia bila utaratibu inakuletea madhara ndo maana watu wanaelekezwa namna ya kutumia ili iwasaidi badala ya kuangamiza.

“Wito wangu watu waishi maisha ya afya, wafanye mazoezi, waondoe msomgo wa mawazo, ulaji wa mlo kamili, wasinywe dawa ambayo haijathibitishwa au kusajiliwa na vyombo vya serikali pia mamlaka za udhibiti iangalie jambo hilini  vizuri watusaidie kudhibiti dawa za nguvu za kiume ambazo hazijafanyiwa utafiti,”alifafanua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles