23.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

Nimefarijika na maendeleo ya viwanda-Waziri Mkuu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipata maelezo kuhusu uzalishaji wa saruji  kutoka kwa Pradeep Punlana  (katikati) ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha saruji cha  Rhino kilichopo eneo la Maweni jijini Tanga  wakati alipotembelea kiwanda hicho Jana.

                                    Bethsheba Wambura

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema amefarijika na maendeleo ya ujenzi wa viwanda kwenye mkoa wa Tanga kwa sababu vitasaidia katika ukuaji wa uchumi na kuongeza ajira.

Hayo yameelezwa jana jioni Alhamisi Novemba Mosi wakati alipotembelea kiwanda cha saruji cha Rhino na kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh, vyote vya jijini Tanga.

Waziri Mkuu ambaye jana alihitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tanga, amewapongeza wawekezaji wa viwanda hivyo kwa kuunga mkono mkakati wa Serikali wa kukuza uchumi kutoka wa chini hadi wa kati ifikapo 2025 kwa kupitia sekta ya viwanda.

Akizungumzia kuhusu kiwanda cha Rhino, Waziri Mkuu alisema kiwanda hicho na vingine vya saruji nchini vitasadia kupunguza gharama ya saruji nchini na kurahisisha ujenzi.

“Serikali inaamini kwamba uwepo wa viwanda mbalimbali nchini si tu utawezesha ukuaji wa uchumi wa Taifa, pia utasaidia katika kumaliza changamoto ya ajira hususani kwa vijana.”

Akiwa katika kiwanda cha Tanga Fresh, Waziri Mkuu aliwataka wafugaji mkoani Tanga wabadili mfumo wa ufugaji na wafuge kwa kutumia njia za kisasa ili waongeze uzalishaji.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama usindikaji wa maziwa wakati alipotembelea kwanda cha Maziwa cha Tanga Fresh cha jijini Tanga, Novemba 1, 2018.  Kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, watatu kushoto ni Meneja Ufundi wa kiwanda hicho, Adam Gamba na wanne kukhoto ni Meneja Mkuu wa kiwanda, Michael Karata.

“Wafugaji lazima wakubali kubadilika watumie fursa ya uwepo wa kiwanda hiki kwa kufuga kisasa ili wapate maziwa mengi kwa sababu wana uhakika wa kuyauza kiwandani hapa”.

Aidha Waziri Mkuu amewataka wananchi walioajiriwa kiwandani hapo wafanye kazi kwa bidii, uaminifu na wawe waadilifu na wasijihusishe na vitendo vya wizi kwa kuwa havina tija.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,183FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles