29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

NIKKI: KUJICHUBUA NI UBAGUZI WA RANGI

NA GLORY MLAY


MKALI wa muziki kutoka kundi la Weusi, Nickson Simion ‘Nikki wa Pili’, amewashangaa watu ambao wanajichubua ngozi, huku wakiwalalamikia Wazungu ni wabaguzi wa rangi.

Msanii huyo amewataka wazazi kuwaelimisha watoto wao juu ya ubaguzi wa rangi pamoja na maisha yao ya baadaye na si kuwaacha wakifanya mambo ambayo hayana maana kwa jamii.

“Tumekuwa na tabia za kuwalalamikia Wazungu kuwa ni wabaguzi wa rangi hasa kwa ngozi nyeusi, lakini tunasahau wale ambao wanajichubua bado wanafanya ubaguzi.

“Kitendo cha kuikataa ngozi yako na kuamua kujichubua ili uwe na ngozi nyeupe ni sawasawa na ubaguzi wa rangi, hivyo haina maana ya kuwashangaa Wazungu wakitubagua juu ya rangi zetu, tunatakiwa tujikubali jinsi tulivyo,” alisema Nikki.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles