26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Nikikutana na Jaji Mkuu nitamwambia haya

Mwandishi Wetu

NATAMANI kukutana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Musa ili nizungumzie naye mambo mbalimbali.

Nasema hivyo nikiwa na sababu zangu kadhaa za kuonana naye kutokana na kazi nzuri inayofanywa na mhimili huu, lakini haitangazwi kwa wananachi ipasavyo.

Tangu alipokabidhiwa jukumu la kuongoza mhimili huu, Jaji Musa amekuwa mhimili mkubwa wa kuleta mageuzi makubwa ambayo tunayashuhudia hivi sasa.

Ni ukweli usiopingika kuna mambo makubwa ambayo yamefanyika ndani ya miaka minne hii, lakini huwa nadra mno kusikia wahusika wa mahakama wakiyatangaza kwa wananchi.

Nasema hivyo nikiamini baadhi ya mambo lazima yafuate utaratibu wa kiofisi, lakini mengine hayana kificho kabisa kwa manufaa ya Watanzania.

Kwa mfano, ujenzi wa mahakama za wilaya, mkoa na mahakama kuu za kanda kazi kubwa imefanyika na inaendelea kufanyika kila kukicha, lakini husikii kama kuna mtu kutoka ndani ya mhimili huu anasimama na kusema tumefanya hili hili na kwa gharama hizi.

Hii ni haki ya wahusika ndani ya mhimili huu kuutangazia umma maboresho haya yote ambayo leo mtu akifika kwenye majengo mapya anabaki amepigwa butwaa. Haya ni mapinduzi makubwa ambayo yanatokana na usimamizi mzuri wa Jaji Mkuu

Nakubalinali na Jaji Mkuu kuwa umefika wakati sasa watumishi na viongozi wa mhimili huu kutangaza maboresho na shughuli mbalimbali zinazofanywa ili zifahamike kwa jamii.

Naamini katika mpango mkakati wa Mahakama ya Tanzania wa miaka mitano kuanzia  2015/16 hadi 2019/20, kumekuwapo na maendeleo makubwa kuanzia utoaji huduma,kesi kusikilizwa mapema, rushwa kupungua hasa mahakama za ngazi ya chini ambazo awali zilizonekana kuwa ‘machinjioni’ kwa wananchi wanyonge.

Lazima watumishi wa mahakama, wawe wabunifu kujitangaza katika maboresho  haya ili mwananchi wa kawaida aliyeko Butiama au Kakonko mkoani Kigoma ajue nini kimefanyika.

Inasikitikisha kuona juhudi hizi zinaiishi kwa watu wachache wakati kazi inafanya usiku na mchana kuboresha huduma.

Hivi mahakama ikijitangaza imefanya hiki na hiki dhambi iko wapi? Mbona Serikali kuu inajitangaza na kila mmoja wetu anakubali kinachofanyika hivi sasa?  Nashauri  viongozi watafute njia ya kujitangaza haraka. Yapo mambo mazuri yamefanyika Kigoma na Sumbawanga,mahakama ziko vizuri na zinavutia mno. Nasema umefika muda wa kubadilika kwa wasaidizi wa Jaji Mkuu.

Jaji Mkuu, amefanikiwa kwa nguvu kubwa kuboresha taasisi hii, mambo ya urasimu yamepungua  au  kuvunjwa na kuweka pembeni tofauti ya vyeo au hadhi, kwani jambo linalopaswa kuzingatiwa ni utaalamu wa mtu.

Jaji Mkuu, napenda kumalizia kwa kusema kazi kubwa unayoendelea kuifanyia inaungwa mkono na Watanzania na kila mmoja wetu anaiona kwa macho yake.

Maboresho makubwa uliyofanya kuanzia kwa mahakimu na majaji kuwekewe viwango usikilizaji wa kesi kwa mwaka, vimeleta manufaa makubwa ya kupunguza mlolongo wa kesi kuchukua muda mrefu.

Ushauri wangu, watumishi wa mahakama naamini mmemsikia kiongozi wenu anasema tafuteni njia ya kutangaza kazi mnazofanya na si kujifungia ndani, zipelekeni kwa wananchi ndiyo wadau wenu kubwa.

0714 207 553

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles